Na Mwandishi wa A24Tv Arusha
Vijana wa UVCCM kata ya Levolosi jijini Arusha,wametishia kurejesha kadi za uanachama wa chama hicho na kujiunga na vyama vya upinzani baada kutoridhishwa na mwenendo wa uchaguzi uliofanyika katika ofisi ya ccm katika kata hiyo.
Wakiongea kwa jazba mara baada ya katibu wa ccm kata hiyo,Aisha Mbaraka kutangaza matokeo,mmoja ya vijana hao,Hasan Ayub alisema kuwa hakubaliani na matokeo hayo kwani wanaami yalipangwa na mshindi aliandaliwa na hakuwa na sifa za kuchaguliwa.
Alisema kuwa mshindi aliyetangazwa,Rasul Ramadhani aliyeshinda kwa kura 19 na kuwashinda wenzake, Hasani abdul aliyepata kura moja na Justine Renatus aliyepata kura 2,hakustahili kuwa mgombea kwa sababu hakuwa na sifa stahiki ikiwemo umri wa mgombea huyo kuwa mkubwa.
“Kwanza wametuletea mabaunsa wakutudhibitu ,walipanga hayo matokeo hatukubali huu ni uonevu wanampitisha mtu ambaye sio mkazi wa Levolosi ”
Naye Justine Renatus alisema kuwa hakubaliani na matokeo ya uchaguzi huo kwa kuwa anaamini yalijaa udanganyifu na mshindi alipangwa na sio mkazi wa kata hiyo na umri wake ni xaidi ya miaka 35 kinyume na katiba inayotaka mgombea lazima awe na umri usiozidi miaka 34.
“Sisi ndio wazaliwa wa Levolosi huyo aliyeshinda hajulikani ni mkazi wa wapi na walimuandaa ,hatukubaliani na matokeo ya kupika tutakata rufaa na tukiona mambo ndo haya haya tunarudisha kadi”alisema Renatus
Aliongeza kuwa amepanga kukata rufaa ngazi za juu na iwapo kama matokeo yatapaki kama yalivyo watarejesha kazi zaccm na kujiunga na vyama vingine vya upinzani.
Hata hivyo katibu na ccm kata hiyo,Aisha Mbaraka ambaye ndiye msimamizi wa uchaguzi huo aligoma kuzungumzia madai hayo hawezi kuongelea chochote kwa kuwa uchaguzi huo ni wa ndani na kwamba yeye sio msemaji wa chama.
Aliongeza kuwa iwapo kama kuna mgombea hakulizika na matokeo hayo anaweza kukata rufaa ngazi husika.
Katibu wa ccm wilaya ya Arusha,Kataba Sukuru aligoma kuzungumzia akisema ni uchaguzi wa ndani.
Uchaguzi huo ni mwendelezo wa chaguzi mbalimbali zinazoendelea ndani chama cha mapinduzo huku leo umoja wa vijana uvccma wakifanya chaguzi hizo katika kata mbalimbali za jiji la Arusha.