Na Geofrey Stephen .Arusha
Mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanga imefanikiwa kuvuka lengo la kuhudumia jumla ya tani 867,00 ikiwa ni Matokeo ya awali mara baada ya uwekezaji mkubwa wa bandari hiyo
Akiongea na waandishi wa habari mapema Leo jijini hapa Msemaji wa bandari hiyo Peter milanzi alisema kuwa uboreshaji huo ulianza toka mwaka 2019.
Milanzi alisema kuwa katika mamlaka hiyo tangu kujengwa kwake,Bandari ya Tanga ilikuwa inahudumia shehena katika kina kirefu Cha maji (Stream Operation)eneo la umbali wa kilomita 1.7kutoka gatini kwa sababu ya changamoto ya kina kifupichq maji eneo la gati amabpi kina Cha maji kilikuwa ni mita 3
Aliongeza kuwa hali hiyo ilikuwa inafanya melu kubwa kushindwa kufika gatini,ambapo kutokana na changamoto hiyo serikali kupitia mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania iliamua kufanya uwekezaji mkubwa ili kutatua changamoto hiyo kwa lengo la kuhudumia meli nyingi na shehena kubwa zaidi.
“Mamlaka husika iliona changamoto hiyo Serikali iliamua kutenga fedha jumla ya Bilioni 429.1 ili kutekeleza mradi mkubwa na WA kimataifa katika bandari ya Tanga na mradi huo wa maboresho ya bandari iliweza kutekelezwa katika awamu mbili”alisema
Milanzi aliendelea kwa kusema kuwa katika awamu hizo Agosti 3 TPA iliingia mkataba wa miezi 12 na kampuni ya china Harbour Engineering company (CHEC)limited na mhandisi mshauri wa mradi ni kampuni ya NIRAS kutoka denrmak ikishirikiana na kampuni ya kizawa ijulikanayo kwa jina la ANOVA
“Awamu hiyo ya kwanza ya mradi ilihusisha uchimbaji wa kina Cha maji kwenye mlango wa kuingilia meli (enterance channel)na sehemu yakugeuzia meli (turning basin)kutoka mita 3 hadi mita 13 pamoja na ununuzi wa mitambo ya bandari (operation equipment)kwa gharama ya shilingi 172.
“Awamu ya pili kumfuatilia utekelezaji wenye mafanikio wa mradi wa utekelezaji wenye mafanikio wa mradi wa maboresho ya bandari ya Tanga na utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 61,mkandarasi tayari ameshakabidhi kipande chenye urefu wa mita 200 hali hiyo imewezesha Bandari ya Tanga kuanza kupokea melu na kuhudumia meli na kuhudumia meli gatini zisizozidi mita 200 kama ilivyofanyika katika bandari ya Dar es salaam.
Mbali na hayo aliwataka wafanyabiashara wa Kanda ya kaskazini kuhakikisha kuwa wanatumia vyema bandari hiyo kwa kuwa mpaka Sasa wameshaiboresha kwenye viwango vya ngazi ya kimataifa
Alihitimisha kwa kusema kuwa wameshafanya mafunzo maalumu kwa wahudumu sanjari na kuwapa mbinu mbalimbali za kibiashara za kimataifa.
Mwisho