Na Geofrey Stephen Arusha .
Katika kuakikisha vijana wanajikwamua katika ajira kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo SERIKALI kwa kushirikiana na Shirika la viwanda vidogo SIDO,kupitia mradi wa wanagenzi , imewawezesha vijana wapatao 130 mkoani Arusha ,kupata mafunzo ya ujasiriamali kupitia viwanda vidogo ,ambayo yamewasaidia kuwapatia ujuzi na uthubutu katika sekta hiyo.
Hayo yamebainishwa na Katibu tawala Rasilimali watu Mkoani hapa,David Lyamongi wakati akifunga mafunzo ya mwezi mmoja kwa vijana hap 130 waliohitimu mafunzo ya viwandani pamoja na kuwatunuku vyeti wanagenzi, iliyofanyika jijini Arusha.
Lyamongi ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongela,alitoa rai kwa wahitimu hao kuhakikisha wanatumia uzoefu walioupa kubuni na kwenda kuanzisha viwanda vidogo vitakavyowasaida kujiajiri na kupunguza janga la ajira hapa nchini.
Katibu tawala huyo alilipongeza shirika la SIDO kwa kutekeleza vema mradi huo unaosimamiwa na serikali kupitia wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia na kufadhiliwa na benki ya dunia ambapo alisema ,serikali inatambua changamoto za vijana.
Awali meneja wa SIDO mkoa wa Arusha,Jafary Donge aliishukuru serikali kwa kukubali kuwapatia mafunzo na mitaji vijana hao ambayo yamesaidia kuwapatia uzoefu mahala pa kazi.
Alisema hadi sasa mradi huo umefanyika katika mikoa 12 na kuwafikia vijana 1647nchini huku mkoa wa Arusha kupitia halmashauri ya Arusha DC,Meru na jiji ukiandikisha vijana 130 wakiwemo wanawake 66.
Alisema kuwa jukumu la SIDO katika mradi huo ilikuwa ni kuratibu vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 35 ambao walihitimu mafunzo ya SIDO na katika taasisi na vyuo mbalimbali.
“Baada ya kuwapata vijana hao tuliwaunganisha na wanagenzi ambao waliwapatia mafunzo katika viwanda vyao kwa muda wa mwezi mmoja huku serikali ikiwapatia kiasi cha sh.100,000 kila wiki kama fedha ya kujikimu “alisema.
Alisema vijana hao walishiriki na kufuzu mafunzo ya uokoji wa mikate,usindikaji wa vyakula,asali na Vipodozi,Utengenezaji wa Sabuni,Ushonaji,Uhandisi, ufundi magari , utalii na Urembo.
Baadhi ya wanagenzi,Ally Babu kutoka kampuni ya uokaji mikate ya Bilsarm ,Irene Baker na Ahmed Abdalah (Dallerz Group)waliipongeza serikali kwa hatua ya kuwapatia mafunzo vijana kupitia viwanda ikiwa ni njia mojawapo ya kukabiliana na wimbi la ajira hapa nchini.
“Mpango huu ni mzuri kwani unatusaidia hata sisi kupata wafanyakazi bora tuliowafundisha wenyewe na pia utasaidia kupunguza wimbi la ajira kwa baadhi yao watakaojiajiri “alisema Irene Manzi anayemiliki Irene Baker eneo la Majengo na Maromboso jijini hapa.
Ends…