Tim ngumu ya Merves Hotel ya jijini Arusha imeangushia kichapo kizito Timu ya Maveteran ya Moshi Dc Goli saba kwa tatu na kuendelea kujiwekea historia ya Timu ngumu katika ukanda wa Arusha inayo toa dozi.
Mechi hiyo ya aina yake iliyo chezwa katika uwanja wa sinoni jijini Arusha na kushughudiwa na maelfu wa mashabiki wa mpira jijini Arusha ilikua ya aina yake kutokana na vikosi kua moto
Akizungumza na A24Tv Meneja wa Timu hiyo Mathayo Peter Kabaa Amesema kwamba timu yake imefanya vyema kutokana na mwendelezo mzuri wa kujifua kuelekea michuano mbali mbali
Kabaa amesema lengo la mashindano hayo ni kuimarisha ulinzi na usalama katika wilaya ya Arusha pamoja na kutangaza biashara ya hotel ya kisasa ya Merves Hotel hilioko Philips Jijini Arusha
Magoli Hayo yamewekwa nyavuni na Laizer ambaye ametikisa nyavu mara tatu mfululizo ,huku magoli mengine yakiwekwa nyavuni na mshambuliaji hatari Cliton Akifunga goli moja ,Joshua goli moja Rasta akifanya kufuru la ya magoli mawili kwa upande wa Merves Sport club .
Huku wapinzani wao wakipata penat moja na mfungaji wa magoli mawili ni Bwana senga .