Na Emmanuel octavian
Halmashauri ya mji wa Njombe inatarajia kutekeleza mradi wa kuboresha mazingira wa Takribani shilingi bilioni 4 kwa mashirikiano na mji wa Miltenburg wa nchini Ujerumani katika miradi miwili ya awali kwa awamu tofauti ikiwemo kubadili taka kuwa rasilimali pamoja na uzalishaji umeme wa jua na kuupeleka kwenye gridi ya taifa.
Hoja hiyo imewasilishwa katika mkutano maalum wa baraza la madiwani la kujadili ufungaji wa hesabu za mwaka wa fedha uliopita ambapo wageni toka nchini Ujerumani wamefika kujifunza namna ya kwenda kutekeleza mradi huo kwa pande zote mbili ambapo nao watakwenda kutekeleza watakayojifunzi katika halmashauri ya mji ikiwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo Erasto Mpete akisema kutakuwa na manufaa makubwa katika kuboresha mazingira.
Sebastian Rundig ni Meneja mazingira katika mji wa Milternburg ujerumani ambaye amesema wanatarajia kujifunza masuala mbalimbali ya mazingira pamoja na kutoa elimu ya matumizi ya umeme wa sola utakaokwenda kuchangia kwenye gridi ya taifa.
Mkuu wa wilaya ya Njombe kissagwakisakasongwa amesema mwezi oktoba wanatarajia kwenda nchini ujerumani kuwasilisha andiko hilo ili waweze kupata fedha hizo huku mwandishi wa mradi huo Emmanuel George ambaye ni katibu tawala wilaya ya Njombe akisema mahusiano mema baina ya halmashauri ya mji wa Njombe na Milternburg ndiyo yamesababisha kuendelea vyema na mradi huo.
Baadhi ya madiwani akiwemo Nestory Mahenge na Tumain Mtewa wamesema endapo mradi huo utafanikiwa basi itakuwa ni fursa kubwa kwa wananchi katika kuboresha mazingira. Kauli mbiu ya kuundea na kuutekeleza mradi huo ni”kuuweka mji katika hali ya kijani na safi.