Na Mwandishi wa A24Tv Njombe
Katibu wa CCM mkoa wa Njombe Julius Peter ameagiza kuvunjwa kwa makundi yote yaliyokuwapo katika jumuiya ya wanawake UWT mkoa wa Njombe kabla ya kufanyika kwa uchaguzi ndani ya chama hicho na kwamba hivi sasa kinachotakiwa ni kuungana kufanyakazi.
Katibu huyo ametoa agizo hilo baada ya kukamilika kwa uchaguzi huo ngazi ya mkoa uliomchagua Scholastica Kevela kuwa mwenyekiti wa UWT pamoja na wajumbe mbalimbali huku akisema anataka kuona kazi zinakwenda na sio kuendekeza makundi.
Baadhi ya wanawake wa UWT akiwemo Esteria Mbwilo,Tumain Mtewa na Neema Mbanga wamesema wanamatumaini makubwa toka kwa Viongozi wao katika kuhakikisha maendeleo yanasonga
Msimamizi wa uchaguzi huo Juma Sweda ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Makete amesema Wajumbe hao wamemchagua Scholastica Kevela kuwa mwenyekiti wao kwa kumpa zaidi ya kura 200.
Baada ya Kutangazwa mshindi katika nafasi ya uenyekiti wa UWT mkoa Bi.Kevela ameahidi kwenda kutekeleza yale wanawake waliyomtuma ikiwa ni pamoja na kuinua uchumi wa wanawake.