Na Geofrey Stephen Arusha
Mke wa Nabii Mkuu Mh GeorDavie Mchungaji Anna Davie ameiomba serikali kutengeneza bara bara ya kuelekea nyumbani kwake iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha Bara bara ya njia ya Likamba . kwani Mtumishi wa Mungu Nabii Mkuu GeoDavie ambayo kwa muda mrefu imekuwa na changamoto ya kupitika hasa kipindi cha mvua .
Akizungumza katika ibada ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Nabii Mkuu Dokta GeorDavie Mchungaji Anna Davie amemuomba Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mrisho Mashaka Gambo kupeleka kilio hicho kwa Mh Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzanai Mh Rais Samia Suluhu Hassan kutambua changamoto hiyo ya barabara ya kwenda kwa Nabii Mkuu GeorDavie ambayo kwa muda mrefu ameiomba serikali kufanyia marekebisho lakini mpaka sasa hakuna kilicho fanyiwa kazi .
Awali Mke wa Nabii Mkuu alimuomba Mbunge wa Arusha Mjini Gambo kufikisha maombi hayo kwa Rais Samia au bungeni kwa lengo la kufanyiwa utekelezaji wa haraka zaidi kwani barabara hiyo hutumika na wananchi kujipatia vipato na wengi wao ni wakulima pamoja na wafugaji .
“Naomba sana Mh mbunge fikisha maombi yangu kwa Mh Rais Mama yetu Samia Suluhu Hassan amjengee baba barabara ya kufika kwake ambayo inatumika na wananchi ambao ni wakulima na wafugaji na wanategemea kusafirisha mifugo yao kupeleka minadani pamoja na kusafirisha mazao yao” Alisema Mchungaji Anna Davie .
Mara baada Maombi hayo Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo alisema amepokea na kufanyia kazi na mara baada ya muda mchache alimjibu mke wa Nabii kuwa atalifanyia kazi mara baada ya kuwasiliana na wataalamu.
Hata hivyo Mbunge wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo alimshukuru Nabii Mkuu Mh Dokta GeorDavie kwa kutumia utajiri wake kusaidia jamii ya chini pamoja na wafanya biashara wa soko la Samunge pamoja na kutoa mitaji kwa kina mama na vijana wa kitanzania ambao kwa asilimia kubwa amegusa na kuwabadilisha katika maisha yao .
Gambo amesema kuwa, toka wafanya biashara wa Samunge wapewe zaidi ya shilingi Millioni Mia moja kwa wafanya biashara wa Samunge wamekuwa na mafanikio makubwa katika biashara zao na uongozi wa somo kwa sasa wameanza ujenzi wa uzio wa soko pamoja na kuweka mageti ya kuingilia sokoni hapo lakini yote hayo ni kutokana na Nabii Mkuu Mh GeorDavie kuwasaidia wafanya biashara hao.
Mwisho .