Matukio katika hafla ya kukabithi piki piki katika kituo cha diplomatic polisi station cha Jijini Arusha na Waziri wa maliasili na utalii Mh Mohamed Mchengerwa kwa jeshi la polisi kitengo cha utalii
Waziri wa maliasili na utalii amekabidhi pikipiki 15 na kutoa ujumbe zitumike katika kazi za serikali ususani kukuza utalii kwa jiji la arusha na viunga vyake
Waziri wa maliasili na utalii Mohamed Mchengerwa akizungumza katika hafla ya kukabidhi piki piki kwa jeshi la polisi mkoani arusha kitengo cha dilpomatic cha utalii
Katika hafla hiyo Mh Waziri amelitaka jeshi la polisi kitengo cha utalii kutumia piki piki hizo katika kazi za utalii kusaidia wageni wanaotembelea mkoani arusha kufanya utalii kutatua changamoto wanazo kutanazo na kutangaza utalii vizuri katika nchi wanazo toka
Piki piki zilizo tolewa na Bank ya CRDB kwa lengo la kukuza utalii katika mkoa wa Arusha
Waziri ameshukuru Bank ya CRDB kwa mchango wake mkubwa wa kurudisha faida wanayo ipata kwa jamii na kutaka kuendelea kugusa makundi mengine muhimu
Maofisa wa jeshi la polisi kitego cha utalii katika picha ya pamoja wakiwa wamevalia nguo pamoja na kofia ngumu katika hafla hiyo ya makabidhiano ya piki piki
Mkurugenzi mtendaji wa bank ya CRDB nchini Abdulmajid Nsekela amesema kwamba bank hiyo imeguswa katika kuelekea katika mkutano wake mkuu wa 28 kutoa piki piki hizo kuunga mkono jitiada za Mh Rais Samia Suluhu Hassan katika sekta ya utalii ya The Royal Tour kwani bank hiyo inashirikiana vizuri na serikali .
Mkurugenzi Mkuu wa Bank ya CRDB NZEKELA akizu gumza katika hafla hiyo ya kukabidhi piki piki hizo kwa jeshi la polisi kitengo cha diplomatic cha utalii jijini Arusha
Mkuu wa Wilaya Arusha Felician Mchengerwa ameshukuru kwa Bank ya CRDB kwa msaada huo wa piki piki na kusema kua wilaya ya Arusha ina mikakati ya kuboresha soko la mbuzi kwa mrombo liwe la kisasa kwa lengo la kuvutia watalii Wanaofika wilayani hapo kufuraiya eneo hilo ambalo limekua kivutio kwa wageni.
Amesema mpaka sasa jitiada zilizo wekwa kuboresha utalii katika mkoa na wilaya arusha unaenda vizuri hivyo wataendelea kushirikiana na viongozi mbali mbali kukuza utalii nchini
Awali Mbunge wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo ameomba kufanyiwa maboresho katika kitengo hicho cha utalii kwani akina adhi ya utalii kwa uapnde wa barabara na kuwekwa pevin kwa china pamoja na kupiga rangi kituo hicho ikiwemo na kumalizia kujenga ukuta wa kumalizia kuzunguka kituo hicho cha utalii.
Maagizo ya Mh Waziri wa maliasili na utalii kuwataka Mamlaka ya Ngoro Ngoro na Tanapa kufanya ukarabati katika kituo hicho pamoja na kuwaagiza halmashauri ya Jiji la Arusha kuptia baraza lake la Madiwani kupitisha bajeti ya ujenzi wa lami kwa kiwango cha lami kwenda katika kituo hicho cha utalii
MWISHO