Na Geofrey Stephen Arusha
Kwa mwaka huu wa 2023 Zaidi ya nchi 30 kutoka Duniani na makampuni zaidi ya 300 zinatarajia kushiriki maonyesho ya Karibu kill fair viwanja vya Magereza kisongo jijini Arusha.
Akizungumza na Vyombo vya habati Mkurugenzi mtendaji wa kill fair promotion limited Dominic Shoo amesema kuwa maonyesho ya karibu Kili fair inauza Tanzania kwasababu ya kutembelea na kutafuta masoko nchi zingine duniani Ili waweze kuonana na watanzania.
Shoo amesema kuwa ongezeko la utalii nchini Tanzania limechangiwa zaidi na kampuni ya karibu kill fair ambapo amesema kmataifa hayo yatakayoshiriki yanatarajia kua na lengo la kuona Tanzania ina nini Ili waweze kuitembelea vivutio vya utalii vinavyo patikana hapa nchini .
Makamu mwenyekiti wa Tato Henry Kimambo amesema kuwa kuwa lengo kubwa la tukio Hilo la maonesho ni kuwezesha kuunganisha wadau wa sekta ya utalii kutoka nchini na nje ya nchi ya Tanzania kupelekea kuungana na mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kuweza kufikisha watalii 500 mkaka kufikia mwaka 2025.
Miongoni mwa wadhamini katika maonyesho hayo Benki ya Crdb nchini imesema kuwa wanajivunia kushiriki katika maonesho hayo kwani lengo la kushiriki ni kulenga kuinua sekta ya utalii,ukizingatia benki ya crdb kuwa benki ya kwanza nchini kwa kuanzisha kadi maalum ya kuwezesha watalii kufanya malipo wakiwamo wafanyabiashara kunufaika na mikopo mbalimbali ya biashara.
Na ijulikane kuwa katika nchi ya Tanzania benki ya serikali ya crdb siyo mara ya kwanza kudhamini maonesho hayo na kulingana na takwimu kutoka benki kuu nchini mwaka2022 baada ya ya biashara ya dhahabu kuingiza pesa nyingi Tanzania biashara inayofuatia ni hii ya utalii ambapo serikali imeweza kuingiza kiasi Cha bilion 2.4 za kimarekani. Hii inaonesha namna ambavyo serikali inapata mapato.
Mwisho