Na Geofrey Stephen Arusha .
Matukio ya kushamiri kwa wivu wa mapenzi mkoani Arusha yaanza kutikisa tena mara baada ya Mwanamke Mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Jackline Mnkonyi{38} mkazi wa Sombetini Jijini Arusha mei 23 mwaka huu majira ya saa 5 usiku alipata kipigo kikali kutoka kwa mume wake ikiwa ni pamoja na kung’olewa meno mawili na kutobolewa jicho kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwa wazazi wake eneo la Sinoni kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha,Jackline alisema kuwa baada ya kupata kipigo hicho alichukuliwa bila kujitambuwa na kupelekwa nyumbani kwa wazazi wake Sinoni na kutupwa getini bila ya kujitambua.
Jakline akizungumza na vyombo vy habri kuhusu tukio lilompata kutoka kwa mume wake
Alisema Mume wake mara baada ya kufika eneo la nyumbani aliwapigia simu wazazi wake na wazazi wake walipofungua geti walimkuta katika hali mbaya na baadae waliamua kumchukua na asubuhiu alipelekwa hospital ya kaloleni kwa matibabu zaidi.
Akizungumza Mkasa huo alisema kuwa,mchana wa mei 23 mwaka huu alitembelewa na mjomba wake ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi{CCM} Simiyu aliyetambuliwa kwa jina la Vicent Matai .
Jackline alisema na kumtaja mume wake kwa jina la ,Isaack Mnyagi Mwalimu na mkazi wa wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro huja baada ya muda wa zaidi ya miezi mitatu na zaidi kuona watoto wawili aliozaa nao na siku hiyo alikuja usiku ghafla.
Muonekano wa Jackline akiwa mzima kabla ya kupata kipigo kuyoka kwa mume wake
Alisema alipofika nyumbani Sombetini maajira ya saa 4.45 usiku aligonga mlango na kufunguliwa na watoto lakini hakutaka salamu na kuingia chumbani na alipomfuata alitoka chumbani.
Jackline alipoona hivyo alimuuliza kulikoni alichoambulia ni maneno mazito na matusi na kuulizwa mchana alikuwa na nani na alimjibu kuwa alikuwa na mjomba wake hatua ambayo alikana na kusema kuwa ni mtu wake na huwa wanafanya umalaya hatua ambayo alipinga lakini alijikutaja akipigwa na ‘’mjeledi’’ mgongoni.
Picha ya Mume wa Jacline aliye mshambulia Mke wake kwa silaa za jadi .
Alisema alijitahidi sana kujieleza lakini ilishindikana na Mume wake Mnyagi alichukua Plaizi kifaa cha gereji na kumwamuru afungue mdomo na kung’olewa jino moja baada ya lingine huku akipata kipigo kikali na kujikuta na maumivu makali hadi jana.
Jackline alisema hatua hiyo aliona kama haitoshi aliamua kuchukua kitu chenye Icha kali na kumtoboa jicho moja ambalo hadi sasa hawezi kuona na kumwambia maneno mazito na mtusi huku akiendelea kupigwa hali iliyomfanya kupoteza fahamu.
Alisema hakujua jinsi alivyofikishwa nyumbani kwa wazazi wake Sinoni Daraja mbili na kutupwa getini kwani nilishtuka nikiwa hospital .
‘’Nimetobolewa jicho na nimeng’olewa meno mawili kwa chombo kinachoitwa Plaiz nina maamuvi makali sana naiomba serikali ichukue hatua dhidi ya mume wake kwani amenifanyia unyama wa hali ya juu’’alisema Jackline
Naye Mzazi wa Jackline,Mzee Elimilis John Mkonyi alisema kuwa baada ya kumpeleka katika hospital ya Rufaa ya Mount Meru na kupata matibabu alikwenda kituo kikuu cha polisi Arusha na kufungua jalada shambuli la kuzulu mwili kesi namba ARS/RB/5416/2023.
Mzee Mkonyi mwenye watoto nane na wajukuuu 16 alisema kuwa mume wa mtoto wake wala hamjui na wala hajawahi kujitambulisha kwake kwa muda wote waliofanikiwa kupata hao watoto wao wawili labda mama maana wao ndio wenye siri juu ya mahusiano hayo.
Mzee Mkonyi alisema kuwa mtoto wake,Jckline aliwahi kumweleza mama yake kuwa mume wake amekuwa na tabia ya kumpiga mara kwa mara lakini yeye hajawahi kuelezwa kwani mtoto wa kike huongea zaidi na mama na hadi sasa hajulikani alipo mara baada ya kufanya tukio hilo la kinyama kwa jamii.
”Niliwahi kumzuia mwanangu asidi tena kwa mume wake lakini hakusikia kwani yeye mtoto na mama yake ndio wasiri wakubwa wa kila kitu kifupi naweza kusema hivyo tu mengine tuiache serikali ifanye kazi yake” alisema Mzee Mkonyi.
Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha,Justin Msejo hakuweza kupatikana kwa simu yake ya kiganjani kuelezea tukio hilo kama mtuhumiwa ameshakamatwa au la kwani simu yake ya kiganjani ilikuwa ikiita bila kupokelewa.
Mwisho.