Mbio za nyika za Haydom Marathon (mwaka 2023) zilizofanyika leo wilayani Mbulu mkoani Manyara zimekusanya Zaidi ya shilingi Milioni 115 kwa ajili ya kuwasaidia wananchi masikini kupata matibabu.
Akifungua mbio hizo leo Mei 27,2023, mkuu wa wilaya ya Mbulu Kheri James amepongeza jitihada za wadau hao kutoka kanisa la Kiinjili la Kilutheri jimbo la Mbulu kwa kuendelea kuiunga mkono serikali katika kuhudumia wananchi.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Kilutheri ya HaydomDr.Pascal Mdoe amesema fedha hizo zitakwenda kugharamia matibabu kwa Wananchi wasio na uwezo.
Amesema fedha zilizochangwa na marafiki kutoka mataifa mbalimbali ni Zaidi ya Shilingi Milioni 32.
Jumla ya fedha zilizopatikana ni shilingi Milioni 116 ambapo Milioni 94 zimeshatolewa na zingine ni ahadi.
Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Flatery Massay ameipongeza Hospitali ya Haydom kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali katika Shughuli za Maendeleo ikiwemo huduma za Afya.
Msaidizi wa askofu Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Mbulu John Nade, amesema kitendo Cha kuwachangia wasio na uwezo ni agizo la mungu na linapaswa kuungwa mkono na watu wote.
Mwenyekiti wa chama cha Riadha mkoa wa Manyara Peter Ingi amesema mashindano kama hayo ni heshima kwa mkoa wa Manyara kwa kuwa yanakwenda kuibua vipaji vpya na kuongeza hamasa katika mchezo huo pendwa mkoani hapa.
Mshindi wa kwanza kilomita 21 Herman Vitali Ginan Sulle aliyetumia muda wa 1:4:47, amepata shilingi 600,000, Mshindi wa pili Shing’ade Ginik amepata 300,000, na wa tatu ni Nestory Steven amejishindia 200,000.
Kwa upande wa Wanawake kilomita 21,Mshindi wa kwanza ni Selina Amosi amepata shilingi 600,000, wa pili ni Tunu Andrea amepata laki 300,000 na wa tatu ni Farida Swalehe ambaye amepata laki 200,000.
Kilomita 10 wanaume, namba moja ni Decta Tezi Force, kapata shilingi 400,000, namba mbili ni John Nahhay aliyepata 200,000 na tatu ni John Joseph aliyepata 100,000.
Kilomita 10 Wanawake aliyeshinda namba Moja ni Anastazia Dolomongo 400,000, namba mbili Nuru Benedicto kavuna laki 200,000 na tatu ni Oliva Francis kapata laki 100,000.
Meneja wa Herman mshindi wa kwanza kilomita 21 kwa wanaume, Tumaini Mathayo Muye ameeleza ratiba ya mazoezi kwamba kwa wiki anafanya mara sita, na jumapili huwa anapumzika.
Jumatatu mbio ndefu,jumanne Spidi uwanjani,jumatano mbio ndefu,alhamisi spidi,ijumaa mbio ndefu, Jumamosi Majaribio kwa kufanya mashindano na wengine.
Amesema Changamoto ni kukosekana wafadhili ambapo mwezi Januari alishindwa kwenda kushiriki Mbio za nyika nchini Australia kwa kukosa Vi