Na Geofrey Stephen Arusha
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale ,serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Simai Mohammed Said amesema ni lazima utamaduni wa asili ikiwemo maajabu ya miti mbalimbali utangazwe ili kuvutia watalii wengi kufika nchini.
Aidha alisisitiza ushirikiano uliopo baina ya nchi ya Tanzania na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kutangaza zaidi vivutio vya utalii vilivyopo katika nchi hizo mbili.
Hayo ameyasema wakati akifungua Maonyesho ya Utalii ya Karibu -Kill Fair 2023 yanayofanyika kwa siku ya tatu eneo la Viwanja vya Magereza Jijini Arusha.
Alisema nchi ya Tanzania imefungua fursa za utalii kutokana na fursa iliyotangazwa kupitia filamu ya Royal Tour ambayo imesaidia nchi ya Zanzibar na Tanzania kwa pamoja kupata watalii wengi zaidi wanaotembelea vivutio vya utalii vikiwemo vya asili.
Alisititiza kila mtanzania anapaswa kuwa balozi mzuri wa utalii kwani serikali imejitahidi kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kusisitiza serikali itaendelea kulinda soko la utalii ili kuhakikikisha watalii wanakuja nchi hizi mbili kwaajilli ya utalii zaidi.
“Rais Samia Hassan Suluhu na Rais wa Zanzibar, Dk Alli Hussein Mwinyi wametangaza Utalii na tunaamini msimu huu wa utalii utaleta ongezeko kubwa la utalii hivyo naomba TRA washirikiane na wadau wa utalii ili kuondoa changamoto wanazokumbana nazo wadau wa utalii nchini”
Alisititiza Zanzibar imechaguliwa kuwa eneo la utalii namba moja kwa Bara la Afrika katika msimu huu wa utalii na hii itasaidia kunogesha utalii kwa Tanzania Bara hivyo kwa tukio hili matarajio ya ongezeko la watalii wataongezeka kwani kutakuwa na Ndege ya moja kwa moja kutoka Ufaransa kuja Tanzania na Tanzania Bara.
Naye, Richard Kayombo kutoka TRA alisema mamlaka hiyo itaendelea kushirikiana na wadau wa sekta ya utalii kama kauli mbiu isemavyo” utozaji kodi kwanjia ya kiungwanana kirafiki” na watazingatia maoni ya wadau hao wa utalii ili kuboresha huduma za kodi.
Alisema utalii ukiporomoka sekta nyingine zitaporomoka hivyo kila jambo linalohusiana na utalii litazingatiwa ili kuhakikisha sekta hiyo inatoa huduma zaidi kwani serikali imekuwa ikisikiliza wadau wa utalii na wadau wengine lakini pia uwepo wa dawati la pamojala utalii TRA itazingatia hilo ili kuboresha huduma za utalii nchini na ongezeko la mapato.
Naye mdau wa utalii kutoka kampuni ya utalii ya Zara , Zainab Ansell alisititiza wadau mbalimbali kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini ikiwemo kupanda mlima Kilimanjaro sanjari na kutembelea hifadhi mbalimbali ikiwemo utalii wa asili unaopaswa kutangazwa zaidi.
Huku,Sastabir Hanspul alishukuru uwepo wa maonyesho hayo kwani yanafungua fursa ya kutangaza aina ya magari wanayotengeneza yasiyoharibu mazingira ambayo ni rafiki katika sekta hiyo ya utalii nchini.
Sisi tuo hapa tumeweka magari yetu tunashukuru Mh rais kwa Royal Tour matunda yake serikali imefanikiwa kupata watalii wengi kutokana jitiada ya Mama Samia the Royal Tour .
Awali Mkurugenzi wa Kilifair Ltd,Dominic Shoo,alisema lengo la maonyesho hayo kutangaza vivutio vilivyopo nchini.
Maonyesho haya yanashirikisha makampuni zaidi ya 370 kutoka nchi zaidi ya 12 duniani hivyo kupitia onyesho hilo wanalofanya kila mwaka wamefanikiwa kuleta watu zaidi ya 500 kutoka mataifa mbalimbali duniani ambao wanaamini wamekua mabalozi wazuri wa kutangaza vivutio vilivyopo nchini.
Moja waekezaji Benson Simpson na Rechel Maduhu katika sekta ya utalii ambao wamekuja na helkopta ya kuraisisha kutembelea mbuga za wanyama pamoja na kupanda Mlima kilimanjro wamewafamisha watanzania pamoja na watalii kutoka nje kwamba wamepata kibali kutoka wizara ya mali asili na utalii kusafirisha watalii hivyo wanakaribisha kufanya utalii wa ndani kwa kutumia helkopta mawasiliano ya www.tropicairkenya.com
Mwisho.