Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Missaile Mussa amesisitiza wakulima na wauzaji wa mbegu nchini kuzalisha mbegu Bora zenye kuongeza lishe Ili kuwa na jamii yenye Afya Bora na kukuza Pato lao sanjari na kulima Kwa tija.
Ameyasema hayo wakati akifungua maonesho ya kibiashara Tari Selian Jijini Arusha yenye kauli mbiu,”Kabiliana na mabadiliko ya tabia nchi tumia teknolojia bunifu za kilimo Kwa uhakika wa chakula na kipato” ambapo aliwakilishwa na Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mali Mkoa wa Arusha Daniel Leiruk.
Aidha amesema imeelekezwa kwamba kilimo kinahitajika kuwa na mchango Kwa mtu mojamoja na nchi Kwa ujumla katika Afya na masoko ya ndani na nje ya nchi ndio maana Serikali imetenga bajeti kubwa Kwa mwaka huu wa fedha 2023 /24 takribani Bilion 970 tofauti na mwaka uliopita bilion 770 Kwa ajili ya kuimarisha miundombinu mbalimbali ya mnyororo wa thamani ya kilimo.
“Kwa hiyo tunapaswa Sasa kuamka na tunaposema kilimo biashara hakikisha hatusemi kilimo cha kujikimu Kwani Sasa tunao wafanyabiashara wadogo waokuwa kwenda kufanya biashara kubwa za kilimo ndio lengo la Serikali na Rais hata watafiti wetu wanatekeleza pia sekta binafsi wanatekeleza tunahakikisha huduma hizi zinawafikia wananchi popote walipo.
Kwa mujibu wa Katibu Tawala Msaidizi Leiruk Amesema kufanyika Kwa maonesho hayo kila mwaka ushirikiano huu ukikuwa Kwa sehemu kubwa kauli mbiu inaakisi Kwa kiasi kikubwa teknolojia bunifu tulizoziona jinsi zinamchango wa haya yote tunayafikia na kutekeleza kama malengo ya Serikali.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa Tari nchini Prof.Geofrey Mkomilo Amesema kwamba maonesho hayo ya 11 ya Tari Selian yamelenga kuweza kukabiliana na malengo ya Serikali kuongeza uzalishaji wa mazao matano makubwa ya kimkakati yakiwemo Mpunga Mahindi Alizeti Ngano na Maharagwe ili kupunguza uagizaji wa Ngano na mafuta ya kula nje ya nchi.
Amesema Serikali imeweka lengo la kuongeza uzalishaji wa mbegu za zao la Ngano kufikia Tani 40 ambapo mahitaji yake nchini ni Tani Milion 1 huku Bado zao Hilo likizalishwa asilimia chini ya10 huku asilimia 90 zikiagizwa Kutoka nje ya nchi hivyo kuhitajika hekta 400,000 za kuweza kulima kufikia ongezeko la asilimia 60 hadi 80 ya mahitaji yote.
“Serikali imejiwekea lengo la uzalishaji wa Zao la Ngano nchini Ili kukidhi upungufu wa Zao hilo kufikia mahitaji ya wananchi ambapo tumekuwa tukiagiza karibu asilimia 90 Kutoka nje hivyo Sasa mipango ya Tari ni kujikita kuzalisha Tani 40 ya mbegu za zao hilo kuwafikia wakulima”
Kwa Upande wake Meneja Masoko wa kampuni ya kuzalisha na kuuza mbegu na zana za kilimo EGT Abdul Abass Amesema kampuni Yao imejikita kuzalisha mbegu Bora sanjari na kuongeza thamani ya mnyororo wa mazao nchi Kwa kuzalisha Kwa ubora mbegu na mbolea Ili kuwafikia wakulima .
Nae Mkurugenzi Mstaafu Taasisi za ESA-ICRISAT na SSA-ICARDA Dkt.Said Silim Amesema wakati uliopo unahitaji kubadilika kwenda na mazingira yaliopo kufikia uzalishaji wenye tija kwa mkulima na kuacha kilimo Cha kujikimu kuelekea kilimo biashara kitakachosaidia nchi kuondoa changamoto za upungufu wa chakula na kuzalisha Kwa tija.