Katibu Mkuu Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohamed Hamis akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya Namba maalumu ya Utambuzi kwaajili ya utoaji huduma.
Mkurugenzi wa TEHAMA Priscus P. Kiwango akitoa ufafanuzi juu ya Namba Jamii kwaajili ya utambuzi wa utoaji huduma kwa mwananchi
Kikao cha kujadili uanzishaji wa namba maalumu kwaajili ya utambuzi kwaajili ya utoaji huduma za serikali kati ya Katibu Mkuu Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohamed Hamis Kilichofanyika Jijini Arusha katika hoteli ya Mountmeru.
Kikao cha kujadili uanzishaji wa Namba maalum kwaajili ya utambuzi kwaajili ya utiaji huduma za serikali kiikiendelea Jijini Arusha.
ARUSHA
Kikao cha kujadili uanzishaji wa namba maalumu kwaajili ya utambuzi ya utoaji huduma za serikali kimefanyika Jijini Arusha kikishirikisha Taasisi nyingine
Kama RITA, NIDA ,UHAMIAJI,ZCSRA -Zanzibar,UTUMISHI
Akizungumza katika kikao hicho Katibu Mkuu Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohamed Hamis alisema siyo kwamba wanaanzisha namba nyingine bali wanafanya utaratibu wa namba hiyo bali watakapomaliza majadiliano watakubaliana iwe inamtambulisha Mwananchi na mgeni yeyote atakayeingia nchini.
Aidha amesema kuwa Lengo kubwa la hizo Taasisi ni kupitia kwa pamoja kwani wamenaanza safari ya uchumi wa kidigital kwa kuunganishwa kwenye mifumo mbalimbali kwa kujadili kwa kiana ,kukubaliana na kupata wasilisho la kuwa na namba moja Jamii
“Tuna safari na niyakuipeleka tanzania kwenye uchumi wa kidigitali, na yapo mmbo mengi ya kufanya ili tuweze kufika kule, ili mwananchi aweze kufanya maendeleo lazima atambulike kwa Namba jamii” Alisema
Aidha Katibu huyo alisema kuwa NambaJamii hiyo siyo kitambulisho kipya bali itamtambua mwananchi tangia anapozaliwa hadi anapoondoka duniani huku ikiwa imesheheni taarifa zake zote kikamilifu
Mkurugenzi wa TEHAMA Priscus P. Kiwango alisema kuwa Namba Jamii hiyo itasaidia kuwa na taarifa zote, kwa namba moja tofauti na ilivyo sasa na hiyo itaepusha usumbufu wa kuwa na mlundikano wa vitamulisho ambavyo ni vya mtu mmoja lakini vinamtambulisha tofauti.
Akijibu swali lililoulizwa na mwandishi Alan Isack sliyetaka kujua Je mpango huu wa kuleta namba hiyo haitaleta mkwamo kutokana na Tanzania bara / Zanzibar kwani kila mmoja ana taratibu zake?: Ndiyo maana ya kunakaa kwa pamoja Taasisi ya Nida,Uhamiaji,Rita,Zcsra na Utumishi, tukubaliane kama serikali kwamba mmoja wao awe ndiye atatoa namba ili mwananchi uweze kupata huduma.
“Kila mwanadamu ana mzunguko wa maisha na kwenye matukio hayo kuna taasisi inawajibika, mf. Hospitali, Rita kwenye vizazi na vifo, Uhamiaji kutambua uraia wa mtu lakini bado baadhi haziongei kwa pamoja ndiyo maana tuunajadili Juu ya Namba Jamii”.alisema Katibu
Uzuri wa Taasisi ya Uhamiaji na NIDA ni Taasisi za Muungano, hivyo sisi tunataka mwananchi apate huduma akiwa kwenye ardhi ya Tanzania bara, au Visiwani,kuna baadhi ya huduma za serikali zinatumia namba ya NIDA na bila hiyo hupati huduma,hivyo wale ambao bado wajisajili au waanze mchakato mapema .
Swali jingine kutoka kwa Calvin Novat aliuliza Hili ni suala la kimfumo, je Tanzania imejipangaje kuingia katika mabadiliko haya ya kimfumo?:
Amesema kwenye masuala ya mifumo,Nchi ya Tanzania imeanza kitambo, na baadhi ya mifumo wapo vizuri ila baadhi ya hiyo mifumo haiongei,wanachokitafuta wakienda kwenye mfumo A,B,na C iwe na utambuzi mmoja ambao majina hayatofautiani
Mwisho