Na Geofrey Stepgen Arusha .
Mamlaka ya udhibiti usafiri Ardhini LATRA mkoani Arusha, imetangaza kumalizika kwa mgomo wa daladala uliodumunkwa takribani siku mbili katika jiji la Arusha na kusababisha adha kubwa kwa wananchi, wafanyabiashara na wanafunzi.
Aidha mamlaka hiyo imepiga marufuku kwa chombo cha usafiri cha Bajaj kufanyabiashara ya kupakia abiria kama daladala badala yake imewataka kufanyabiashara hiyo kwa kukodishwa na sio kwenda wakiokota abiria.
Akiongea na vyombo vya habari afisa mfawidhi Latra mkoa wa Arusha, Joseph Michael, amewahakikishia wananchi kuwa hakuna mgogoro wowote kwa sasa baina ya daladala na bajaj na tayari vituo vipya 50 vya daladala vimepangwa kutumika kupakia na kushusha abiria.
Aidha amesema hadi sasa ni babaj 700 pekee zenye leseni ya Latra zinazoruhusiwa kufanya biashara ya hiyo na kwamba bajaj zisizo na leseni hiyo hazitaruhusiwa na zitakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria iwaponitaonekana zinadanyakazi kinyme cha sheria
Pia Latra imepiga marufuku magari yote madogo aina ya haice kuingia mjini na abiria na gari zinazoruhusiwa kubeba abiria mjini ni magari makubwa aina ya coster na kuanzia jumatatu hatua kali zitaanza kuchukuliwa.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Arusha ,waliohijiwa wamepongeza uamuzi wa Latra kupanga vituo vipya vya daladala na pia kupiga marufuku daladala ainanya haice kupakia abiria mjini kutokana na usumbufu unaosababisha msongamano mjini.
Hamidu Nasari mkazi wa mbauda alisema uamuzi huo unalenga kuboresha usafiri katika jiji la Arusha na utasaidia kuondoa msongamano unaosababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wengine wa barabara.
Mwisho .