Na Richard Mrusha, mbeya
Wito umetolewa kwa wananchi hususani wakulima pamoja na wafanyabishara katika Mkoa wa Mbeya kuendelea kujitokeza kwa wingi kwenye banda la Brela katika maonesho ya kimataifa ya Kilimo Nane nane 2023 ili kusajili biashara zao pamoja na makampuni.
Mkuu wa kitengo cha uhusiano BRELA Roida Andusamile amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lake katika maonesho hayo.
Mkuu huyo wa kitengo cha uhusiano BRELA amesema kuwa zaidi ya watu 150 tangu kuanza kwa maonesho hayo kwenye viwanja vya John Mwakangale tarehe 1,8,2023 wamejitokeza kusajili majina ya biashara zao pamoja na majina ya kampuni.
“Nahamasisha wananchi na wadau wengine waendelee kufika kwenye banda hili ili kupewa elimu lakini kusajili majina ya biashara zao BRELA,”amesema Roida Andusamile mkuu wa kitengo cha Uhusiano BRELA.
Amesema kuwa BRELA ni mdau mkubwa wa sekta ya kilimo nchini na kutumia fursa hiyo kuwataka wafike kwa wingi kwenye banda hili ili kupata huduma pamoja na mambo mengine.
Maonesho hayo ya kilimo yenye kauri mbiu isemayo
“Vijana na wanawake ni msingi imara mifumo endelevu na chakula” yanayotarajiwa kufungwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kesho Agost 2023.
Mwisho.