Na Geofrey Stephen Arusha
Mkurugenzi wa Kampuni ya Avat Consultant bi.Edah Mwanry amepongeza Jitihada mbalimbali zilizowekwa katika Uwekezaji wa Vipaji vya Watoto katika Shule ya Msingi ya Enalepo Ili kuhakikisha kuwa wanafikia ndoto zao .
Bi.Mwanry ameyasema hayo katika mahafali ya 15,iliyofanyika shuleni Darajambili katika halmashauri ya Jiji la Arusha.
Amesema kuwa Uwekezaji wa mazingira mazuri ya shule bado hautoshi katika kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaendelea vizuri kitaluma bali Msingi mzuri unaowekezwa kwao kitaaluma.
Akiwatunuku Vyeti wahitimu hao, Mgeni rasmi Bi.Mwanry amewataka wazazi na walezi kuzungumza na watoto wao,wanaohitimu darasa la Saba Kwa kuwa kuna changamoto kubwa ya Maadili katika Dunia ya Sasa ikiwemo swala la ndoa za jinsia Moja.
“Dunia ya sasa imekumbwa na changamoto nyingi sana hivyo wazazi na walezi msisite kuongea na watoto Hawa kuhusu umuhimu wa Maadili na kuhakikisha kuwa kila kitu mtoto anafahamu na ayasikie kutoka Kwa mzazi wake au mlezi.”alisema Bi.Mwanry
Nae Mkurugenzi wa Shule hiyo ya Enalepo Pre and Primary School Bw.Lasaru Sabore ameeleza kwamba wanafurahia uwekezaji wa kusogeza elimu kwa jamii inayo wazunguka,Kwa kuhakikisha kuwa wanatoa elimu bora katika kata hiyo ya daraja mbili Ili kuwezesha wanafunzi kupata huduma hiyo kwa ukaribu.
Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa Shule hiyo ya Enalepo Pre and Primary School Bw.Joseph Muruga amesema anashukuru wamiliki wa shule hiyo kwa ushirikiano ambao wamekua wakimpatia katika kutatua changamoto za kielimu shuleni hapo, na kuakikisha wanafunzi wanapata Elimu Stahiki .
Afisa Elimu Kata ya Daraja Mbili bi.Yuster Njau amesema wana imani kubwa na wahitimu wa darasa la saba katika shule ya Enalepo,kutokana na wanafunzi kufanya majaribio mbali mbali katika kujiandaa na mtihani wa mwisho wa kumaliza darasa la saba .
Bi.Doris Samson Sabore akizungumzia shule yake amesema mafanikio walio nayo yametokana na mshikamano kuanzia waalimu pamoja na uongozi wa shule kushirikiana kwa pamoja katika kutoa elimu bora,ambacho ndicho kipimo cha kufikia mafanikio.
Ameeleza wanatarajia kupata ufaulu mkubwa kutoka kwa wahitimu 33,ambao ukilinganisha na hapo awali wahitimu walikua 12 kwa mwaka 2008 ambao wote walichaguliwa kuingia kidato cha kwanza kwa mwaka 2009.
Mwisho