- Na Geofrey Stephen.
Baraza la Taifa la Hifadhi za Usimamizi wa Mazingira NEMC limetishia kukifunga kiwanda cha kuzalisha virutubisho vya mifugo cha CHANZI kilichopo Njiro jijini Arusha, kutokana na harufu mbaya na kali kwa wananchi wanao ishi katika eneo la njiro viwandani jambo ambalo linasababisha athari za kimazingira na afya kwa jamii. Inayozunguka kayika maeneo ayo .
Baraza hilo limetoa siku saba kwa mmiliki wa kiwanda hicho kudhibiti harufu hiyo na baada ya muda huo kumalizika bila utekelezaji, NEMC itachukua hatua kali ikiwemo kukipiga faini ama kukifunga kufanya uzalishaji .
Akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika kiwanda hicho,kaimu mkurugenzi wa uzingatiaji na utekelezaji wa sheria NEMC Dkt Thobias Mwesiga amesema ni mara ya pili kwa NEMC kufika kiwandani hapo na kutoa maelekezo ambayo yamekuwa hawatekelezwi na badalayake wananchi kuendelea kupata adhari kubwa ya arufu mbaya inayo toka kiwandani hapo .
Kaimu Mkurugenzi Dkt Thobias Mwesiga akizungumza na vyombo vy habari katika kiwanda hicho
“Kama tukija tena kwa mara ya tatu tukakuta bado malalamiko ya wananchi wanaozunguka maeneo haya yanaendelea, tutawapiga faini au kukifunga kiwanda kabisa ili waweza kuchukua hatua hadi hapo tutakapojiridha wameondoa tatizo”
Aidha dkt Mwesiga aliagiza halmashauri ya jiji la Arusha kukamilisha haraka mchakato wa kukihamisha kiwanda hicho kutoka kwenye makazi ya watu ili kunusuru wananchi wanaoendelea kuathirika na harufu mbaya na kali inayotoka kiwandani hapo.
Alisema kuwa NEMC imekuwa ikitoa maelekezo kadhaa kwa mmliki wa kiwanda hicho juu ya malalamiko ya wananchi kuhusu harufu kali na kwamba mara ya mwisho walimwandikia barua mei 23 mwaka huu ya kurekebisha kasoro, lakini ameshindwa kutekeleza na ndio maana wamelazimika kufika tena kiwandani hapo na kutoa onyo la mwisho .
Dkt Mwesiga alifafanua kuwa lengo la Baraza sio kufunga kiwanda ila ni kumwelimisha kwanza mzalishaji na baada ya hapo kama bado ameshindwa kuzingatia masharti hatua kali tunachukua ndio maana tupo hapa.
Naye afisa mazingira wa jiji la Arusha Sigfrid Mbuya alisema halmashauri ipo katika hatua ya mwisho kukamilisha mchakato wa kumpatia eneo jingine mmiliki wa kiwanda hicho aweze kukihamisha katika makazi ya watu.
Alisema kuwa kiwanda hicho kimekuwa msaada mkubwa kwa jiji la Arusha kwa kukusanya taka nguvu takribani tani 25 na kuzigeuza fursa ya ajira kwa kuzalisha virutubisho vya mifugo na bioges .
Hata hivyo alisema pamoja na nia njema ya kiwanda hicho, athari za kiafya kwa wananchi ni kubwa hivyo halmashauri kupitia vikao vyake inakamilisha mchakato wa kuwapatia eneo hilo ili kukiondoa kiwamda hicho katika makazi ya watu.
Naye meneja uzalishaji wa kiwanda cha Chanzi ,Mayasa Mhina alisema kuwa changamoto ya harufu mbaya na kali inayoyoka kiwandani hapo sio ya kila siku ila imesababishwa na kukatika mara kwa mara kwa nishati ya umeme.
Alisema kiwanda hicho kimekuwa kikikusanya takribani tani 25 ya taka ngumu kwenye masoko ya mjini hapa na lengo ni kufikisha tani 65 kwa siku jambo ambalo wanaendelea kuimarisha uzalishaji.
Alisema wapo mbioni kutumia teknolojia mpya kutoka nchi jirani ya Kenya itakayosaidia kuondoa harufu kali za taka na wataanza kuitumia kwa sasa wakati wakisubiri mchakato kukamilika wa kuhamisha kiwanda hicho.
Ends…