Na Geofrey Stephen ,Arusha
Katika kuweka Jiji la Arusha katika hadhi ya Kitaifa na Kimataifa Jiji hilo sasa litawekwa taa katika barabara zote na kufungwa CCTV Camera lengo ni kuweka Jiji la Arusha katika hali ya ulinzi na usalama kwa nyakati zote
Diwani wa kata ya Daraja mbili Prosper Msofe akionyesha ishara ya kupokea maelekezo kwa mkuu wa wilaya arusha felician Mtehengerwa
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Filician Mtehengerwa katika Mkutano wa hadhara katika kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha ikiwa ni moja ya mikutano yake katika kata za Jiji hil kutatua changamoto ya vibaka wezi katika kata ya Daraja mbili .
Mtehengerwa alisema Jiji la Arusha linaitwa Geneva ya Afrika hivyo basi sifa hiyo inapaswa kwenda na uhalisia na kutokana na hali hiyo serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni moja katika kufunga taa katika barabara zote za Jiji hilo.
Mkuu wa wilaya arusha felician Mtehengerwa akizungumza na wananchi wa mtaa wa ally nyanya kata ya dara mbili jijini arusha
Alisema mbali ya serikali kutenga fedha kwa ajili ya taa pia serikali imetenga fedha nyingine kwa ajili ya kufunga CCTV Camera katika mitaa yote ya Jiji la Arusha ili wenye kufanya uhalifu waweze kuchukuliwa hatua haraka iwezekanavyo.
‘’Tunataka mama akisahau beki lake au akidondosha kalamu apelekewe na sio kuchukuliwa na vibaka sasa watafute kazi nyingine maana serikali imejipanga’’alisema Mtehengerwa.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kuhakikisha wanapata mwekezaji mwenye vyombo vya kisasa vya kuzoa taka na kuchakata na sio mwekezaji wa kuzoa taka na kwenda kutupa katika dampo kwani stahili hiyo imepitwa na wakati kwa hadhi ya Jiji la Arusha.
Alisema haiwezekani Jiji la Arusha kila kona majalala ya matakataka hilo sio sawa mwekezaji mwenye vyombo vya kisasa anapaswa kupewa kazi hiyo na ifike wakati Madiwani wawajibike katika kumsaka mwekezaji huyo.
Mkuu huyo alisema jukumu hilo sasa liko mikononi mwa Madiwani kushirikiana katika kumsaka mwekezaji mwenye sifa ikiwemo uwezo wa kuchakata takataka na kuzifanya kuwa mbolea kwa wakulima na Jiji linapaswa kuendeshwa kisasa kulingana na hadhi yake.
‘’Jiji la Arusha ni Geneva ya Afrika hivyo basi jina hilo linapaswa kwenda na uhalisia wake kwa kuwa na taa katika barabara zote,kufungwa CCTV Camera katika kila kona na kuwa na magari ya kisasa ya kuchakata taka ‘’ alisema Mtehengerwa
Akizungumzia ulinzi alisema kata inayoongoza kwa uhalifu katika Jiji la Arusha ni kata ya Daraja Mbili hivyo amewataka wazazi kuwaonya watoto wao vinginevyo wasimfuate kwa lolote litakalowatokea.
Amesema daraja mbili hususani mtaa wa ally Nyanya umekisiri matukio makubwa ambayo yamesababisha wananchi kulala mapema kutokana na kupigwa mapanga kuibiwa vifaa vya garama na muda mwingine kuchomwa vizu.
Felician ametangaza vita kwa makundi matatu wakiwemo tatu mzuka vibaka pamoja na wafanya biashara wanuza madawa ya kulevya , na pombe haramu ya gongo hatua kali zitachukuliwa kwa wafu hao .
Mtehengerwa ametoa mwezi mmoja kuhakikisha zinapigwa kura ya kuwataja wahalifu wote wa kata hiyo kuchukuliwa hatua kwani kata ya Daraja Mbili imekithili kwa uhalifu na serikali haiwezi kuliacha hilo.
Naye Diwani wa kata hiyo,Prosper Msofe alimwomba Mkuu wa Wilaya kutoa ushirikiano na baadhi ya viongozi wa kata hiyo akiwemo Mtendaji wa kata John Joseph kuthibiti wahalifu kwani kata hiyo ina vijana wenye sifa mbaya ya uhalifu.
Mbali ya hilo alitoa shutuma ya ofisini ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Ally Nyanya ,Omary Shekh kuwa imejaa rushwa hivyo aliomba vyombo vya dola vinavyohusika kuchukua hatua dhidi ya watendaji wa ofisini hiyo kwani hakuna mwananchi anayepewa huduma bila kutoa rusha ya sh 5,000.
Hata hivyo tuhuma hizo zilijibiwa hapo hapo na Mwenyekiti wa mtaa huo Omary Shekh aliyetambuliwa kwa jina la shekh kuwa tuhuma hizo sio za kweli bali zina lengo la kuwachafua viongozi wa serikali wa mtaa huo kwani wanashirikiana vyema na wananchi katika kuleta maendeleo.
Mwisho