Na Richard Mrusha Geita
Waziri WA NCHI ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Dkt. Selemani Jafo amelipongeza Shirika la madini la taifa STAMICO kwa kutekeleza kwa vitendo maagizo aliyoyatoa wakati wa Maadhimisho wa Miaka 50 tokea kuanzishwa kwa STAMICO ya upandaji miti
Wakati wa maadhimisho hayo STAMICO walikuja na Kampeni ya STAMICO na Mazingira at 50! kwa lengo la kuhakikisha pamoja na uendeshaji wa shughuli za uchimbaji wa madini lakini kuhakikisha mazingira yanatunzwa kikamilifu.
“Nawashukuru sana STAMICO kwa kutekeleza kwa vitendo maagizo yangu ya upandaji miti nimeambiwa mpaka sasa mmeshapanda miti 1650 katika Mkoa wa Dodoma na Geita ni jambo zuri sana.”
Mimi nilifanya ziara bila kuwambia kwa kutembelea eneo la ipagala kuona kama kweli mmetekeleza kwa vitendo maelekezo nimekuta kweli mmetekeleza yote kwani niliona mmezungushia uzio na miti inaendelea vizuri sana.” amesema Dkt Suleiman Jafo.
Aidha Mhe Waziri ameshukuru Shirika kwa kufanya kazi kwa pamoja na vikundi mbalimbali Kama vile Kikundi cha Wanawake na Samia nimeambiwa mliwapa kazi ya kupanda na kutunza miti hapa EPZA miti 560 na miti hii inazidi kustawi vizuri na mmeenda mbali zaidi na mmeweza kuwapa uwakala ya Kuuza Nishati Mbadala ya Kupikia kwa Mkoa wa Geita, kweli Stamico umeupiga mwingi amesema Mhe Dkt. Jafo.
Katika tukio la upandaji miti jumla ya miti 340 iliweza kupandwa na , Mhe Jafo na Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde, Grace Kingalame Kaimu Mkuu wa mkoa wa Geita na mkuu wa wilaya ya Nyang’wale pamoja na viongozi wengine wa chama na Serikali wameshiriki katika shughuli hiyo ya kupanda miti.
Miti hiyo imepandwa katika Viwanja vya Bomba mbili (EPZA) ambako maonesho ya 6 teknolojia ya madini 2023 yanaendelea na wameshiriki watu mbalimbali zikiwemo taasisi za serikali na mashirika
Mwisho .