Na Richard Mrusha Geita
WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) katika mwaka wake wa fedha 2023/2024 inatajia kujenga jengo la ghorofa la biashara na makazi katika Mkoa wa Geita.
Akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Geita mjini Constantine Kanyasu alipotembelea katika banda hilo katika maonesho ya sita ya tekinolojia ya madini yanayaofanyika katika viwanja vya EPZA
bombambili halmashauri ya mji geita ambapo mbunge huyo alitaka kujua endaopo nje ya miradi ya Serikali wakala hao kama wana mpango wowote wakuwekeza miradi kama hiyo Mjini Geita.
Akijibu swali hilo
Kaimu Meneja Mawasiliano na Masoko – TBA ,Fredrick Kalinga amesema tayari eneo limepatikana ambapo wanatarajia kujenga ghorofa ambapo juu itakuwa kwa ajili ya makazi ya watu na chini kuwa eneo la biashara.
“Mheshimiwa mbunge bajeti ya mwaka huu tunatarajia kujenga jengo la ghorofa pale eneo la round about maarufu msikitini na taratibu zote zimekamilika na muda wowote tutaanza ujenzi wake “amesema Kalinga
Kwakufanya hivyo itakua nafasi nzuri ya kuendeleza majengo mengi zaidi na tunatarajia taasisi zitaongezeka,hivyo sekta binafsi muda si mrefu waarifiwe namna gani watashirikiana na sisi TBA”ameongeza Kalinga
Kalinga ameongeza kuwa kuna miradi mbalinbali ambayo inatekelezwa na mingine ipo tayari imekamilika kama hospital ya rufaa Chato,hospital ya rufaa ya mkoa na majengo ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa .
Aidha ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya sita kwa kuona haja ya kuhuisha Sheria iliyoanzisha TBA kwa kuiboresha kupitia GN namba 595 ya tarehe 25 Agosti 2023 ambayo inairuhusu TBA kushirikiana na Sekta Binafsi kuendeleza miliki nchini kujenga nyumba za kupangisha na kuuza kwa wananchi wote hivyo TBA wanatalajia kujenga nyumba nyingi na kuziuza.
Kwa upande wake mbunge huyo wa Geita mjini amewapongeza TBA kwa kazi nzuri wanazozifanya na kuwakaribisha katika uwekezaji mbalimbali mjini humo.
Mwisho .