Na Geofrey Stephem Arusha
Wiki ya Azaki Jijini Arusha Mchungaji wa Kanisa la KKKT Richard Hananja amevunja ukimya juu ya matukio makubwa ya ukatili juu ya wanawake na watoto jambo ambalo limeleta sinto Fahamu kwa wana ndoa kupelekea kufanyanyiana mauwaji ukatili na kupoteza maisha huku familia zao zikibaki na malezi ya upande moja au kukosa kabisa malezi
Akizungumza na wadau wa wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Mchungaji Hananja amesema matukio ya wanawake kupoteza maisha kisa mapenzi , ndoa kuvunjika kwa sasa yanaonekana ni fashen jambo ambalo limeonekana jamii kukosa mahadili pia kujiweka mbali na Mungu.
Mpaka sasa Ripoti iliyo zinduliwa katika mkutano wa Asasi za kiraiya imeeleza kwamba mauaji ya wanawake Kwa muda wa miaka mitano imeeleza kwamba jumla ya wanawake 2,438 wameuawa kwa mafatizo ya mapenzi na kuacha familia zao yatima kwa kukosa malezi bora ya pande zote mbili yaaani baba na mama .
Mkurugenzi wa kituo cha Haki za Binadamu Dkt . Anna Henga amesema matokeo ya utafiti huo umehusisha pia jeshi la polisi kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ikionyesha wastani wa wanawake 492 waliuwawa kila mwaka na wanawake 43 waliuawa kila mwezi katika kipindi hicho.
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi kwa Mtoto dhidi ya usafirishaji haramu wa binadamu, Tulibake Kasongwa amesema Serikali imeanzisha madawati ya jinsia 420 katika vituo vya Polisi nchini ili kukabiliana na matukio kama hayo hali iliyopelekea mauaji ya wanawake kupungua kwa asilimia mbili kutoka vifo 305 hadi 298 kati ya mwaka 2020 hadi 2023.
Mkuu ameshukuru waandaji wa mkutano huo wa azaki za kiraiya kuwakutanisha kwa pamoja katika kuzungumzia changamoto ma maemdeleo ya azaki nchini kwani wamekua na msaada kubwa kwa jamii ambazo wamekua wakipatiwa msaada na mashirika yasikua ya kiserikali.
Amesema lengo la kutetea wanyama pori pamoja na misitu ni kuakikisha kwamba vizazi vijazo wanakuta rasimali za Tanzania zikiwa sehemu ya vivutio kwani baadhi ya rasimali za nchi kukosa utetezi ni hasara kwa mashirika kama Tanapa na Ngoro ngoro ambao ndio waifadhi wakuu wa wanyama na misitu
Wiki ya azaki inategemea kufikia kilele chake siku ya ijumaa ya october 27 katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Simba hall, Aicc Jijini Arusha baada ya wadau wa taasisi mbali mbaliki kudumu kwa muda wa siku tano wakiwasilisha mada mbali mbali kuhudu maendeleo ya azaki nchini na Duniani kwa ujumla
Mwisho