Na Richard Mrusha
Kampuni ya SUMAJKT Bottling co. Ltd, inayozalisha maji ya Uhuru Peak Pure Drinking Water, imezindua mikondo miwili ya uzalishaji maji na Muonekano mpya wa chupa za maji ya Uhuru Peak,
Akizungumza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali CDF Jacob John Mkunda wakati wa uzinduzi wa mikondo miwili ya uzalishaji maji, amesema Serikali ina matarajio makubwa na Jeshi la kujenga Taifa JKT na Jeshi la wananchi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatambua na kutembea kifua mbele kutokana na mchango mkubwa unaotokana na shughuli wazifanyazo jeshi hilo hasa katika swala zima la malezi kwa vijana.
Jenerali Mkunda amesema kutokana na Serikali kutambua Mchango huo umeweza kulipatia Jeshi hilo Suma Jkt mradi wa ujenzi wa nyumba 5000 dodoma na Mradi wa kulinda bomba la Mafuta hoima.
CDF Mkunda ametoa wito kwa Shirika kuendelea kubuni mikakati zaidi na kuboresha bidhaa ziweze kukidhi soko la ndani na nje ya nchi kwa kuzingatia ubora wa maji ili wateja wafurahie na kuongeza mapato.
Amewataka pia kuendelea kufanya kazi kwa weledi na bidii na kuitunza Miundo mbinu na kufanya biashara hiyo kwa faida na sio kwa hasara.
Akizungumza Mkurugenzi Mtendaji JKT Kanali Petro Ngata amesema kuwa uwepo wa Mikondo hiyo ya uzalishaji maji utaongeza wigo katika Sekta ya maji biashara na ongezeko la wateja katika biashara ambapo utaongeza mapato.
Amesema mkondo wa kwanza unazalisha maji ya 350ml,600,1.6lita,1lita na unauwezo wa kuzalisha lita 10,000 kwa saa.
Na mkondo wa pili una uwezo wa kuzalisha chupa za maji 500 kwa saa na unazalisha maji lita 13,na lita 18.
Nae Mkuu wa tawi la utawala Jkt Brigadier Jenerali Hassan Mabena akimwakimwakilisha Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajab Mabele amesema kiwanda hicho kilianza uzalishaji Mwaka 2018 na kwa kuona kuwa uzalishaji wake ni mdogo ndipo wakaamua kufanya maboresho ili kukiongezea uwezo katika uzalishaji kwa kuongeza mitambo miwili ya uzalishaji yenye uzalishaji unaoanzia Mils 360,600,lita 1,lita1.6,lita 13 na lita 18.
Mwisho .