Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha imemhukumu kifungo cha maisha jela mfugaji, Ole Sure Miliari(19) mkazi wa wilaya hiyo,baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumlawiti Mwanafunzi wenye umri wa miaka 8 na kumsababishia kutokwa damu nyingi sehemu zake za siri.
Kesi hiyo namba 16 ya mwaka ,2023 Miliari alitenda kosa hilo katika wilaya hiyo kwa kumlawiti mwanafunzi huyo ambapo mara baada ya uchunguzi wa Daktari iligundulika aliharibiwa vibaya katika maumbile yake nakupelekea kufungwa nepi (Pampas) kutokana na kitendo hicho cha kinyama .
Akisoma hukumu hiyo jana Oktoba 5,2023 Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo ,Magreth Mboya alisema kuwa Miliari amekutwa na hatia baada ya kuridhishwa na ushahidi wa upande wa Jamhuri na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo na mtuhumiwa kukutwa na hatia hivyo mahakama imemhukumu kifungo cha Maisha jela.
Hakimu alisema mahakama imetoa adhabu hiyo ili iwefundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo isiyokubalika katika jamii ya mtanzania .
Naye Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Mimutie Women Organization , Rose Njilo amesema kuwa wao kama taasisi ya kutetea haki za wanawake na watoto wameishukuru Mahakama hiyo kwa kutenda haki kwani adhabu hiyo itarudisha maadili kwa jamii na kuwa fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo .
Njiro alilishukuru Jeshi la Polisi kwa ushirikiano wao ambao ulifanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa na kufikishwa mahakamani .
Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa jamii kuachana na vitendo vya ukatili na ulawiti hasa hasa katika jamii ya kifugaji ambayo inaonekana kudumisha maadili ya kitanzania ikilinganishwa na baadhi yao kuingia katika vitendo hivyo kinyume na maadili .
Pia ametoa shukrani zake kwa taasisi ya Women Fund Tanzania kwa kuendelea kuwa wawezeshaji wa shirika la Mimutie katika kuibua Changamoto za Ukatili wa kijinsia ndani ya jamii ya Tanzania .
Wadau mbalimbali na wanaharakati walifika katika mahakama hiyo kusikiliza hukumu hiyo na kusema kwamba Mahakama hiyo imetenda haki hasa baada ya mshtakiwa kukiri makosa na hivyo kuitahisishia kazi mahakama hiyo.
Ends…