MAMLAKA ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Nchini (DCEA) imesaini mkataba wa ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi Katika kudhibiti uchepushwaji wa kemikali bashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya ikiwa ni hatua ya kupanua wigo wa kudhibiti ongezeko la dawa hizo Nchini.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kukevya (DCEA) Aretas Lyimo alisema kundi la vijana wasomi wa vyuo vikuu ndio linaloongoza kwa matumizi makubwa ya dawa za kulevya ikiwemo uchepushwaji wa kemilaki bashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya.
Lakini pia taarifa ya hali ya dawa za kulevya Duniani kuanzia mwaka 2017 hadi 2021 zinaonyesha kuwepo kwa matumizi na usafirishaji haramu wa dawa tiba zenye asili ya kulevya matharani dawa tiba zenye udhibiti maalum zilizokamatwa zikisafirishwa kwa njia haramu katika kipindi hicho
Mkataba huo imesainiwa jana kwenye Ukumbi wa jengo la Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,NCAA,Jijini Arusha kati ya Kamishina Jenerali wa mamlaka hiyo Aretas Lyimo na sekta binafsi kama hatua mojawapo ya kudhibiti kemikali bashirifu na dawa tiba zenye athari za kulevya.
Kamishina Jenerali Lyimo,alisema kutokana na kuongezeka kwa tatizo la kutengeneza dawa za kulevya duniani ikiwemo utengezaji wa dawa mpya Kwa kutumia kemikali bashirifu na kushamiri kwa uchepushwaji wa dawa tiba zenye asili ya kulevya ambazo ni Fentanyl,Ketamine,Pethidine, Tramodol,na nyinginezo.
Kamishna Jenerali Lyimo alisisitiza kuwepo kwa wimbi kubwa la Vijana wanaotumia kemikali hizo na kuharibika kiafya na kiakili.
Alisema vijana wasomi wanatumia dawa za kulevya na kuharibika kiafya na kushindwa kupata watoto na huko mbeleni wanaweza kubaki wazee pekee na kusababisha ajira za wasomi kuchukuliwa na wageni kwasababu ya ukosefu wa vijana wasomi
“Tumefanya utafiti mdogo na tumegundua vijana wasomi wanaongoza kwa matumizi ya dawa za kulevya na pia wengine wanasoma nchini Marekani na wengine vyuo vikuu hapa nchini na nchi nyinginezo,tutakosa wataalam wasomi badae sababu ya matumizi ya dawa tiba zenye asili ya madawa ya kulevya”
Alisema athari ya matumizi ya dawa hizi ni kubwa na mwisho wa siku wageni kutoka nje watashika nafasi hizi sababu hatuna wataalam katika fani nyinginezo sasa nawasihi nyie mnaouza kemikali muwe makini ili kudhibiti matumizi ya madawa haya.
Alisema Katika kipindi cha mwaka 2027 Hadi 2024 mamlaka imefanikiwa kuvunja mtandao wa usafirishaji haramu wa dawa za Ketamine zenye uzito wa kilo 450 Kutoka nchi za Ulaya kuja Nchini Kwa kutumia vibali vya kughushi.
Alisema kuwa utafiti uliofanywa mwaka 2021 na bodi ya kimataifa ya kudhibiti dawa za kulevya INCB umezitaja nchi tisa za mfano wa ushirishaji Sekta binafsi kuwa ni Australia,Canada,China, Ufaransa,Ujetumani,India, Uswis,Marekani na Tanzania .
Alisema kuwa taarifa ya dawa za kulevya duniani kuanzia mwaka 2017 hadi 2021 zinaonyesha jumla ya tani 298.8 za dawa ya Tramadol,tani 260 za Morphine tani 33.5 za Fentanyl,tani 6.6 za Benzos ,tani 5.6 za Ketamine,kilo 352.4 za Barbiturates zilikamatwa ,ambazo zilikuwa zikipelekwa,Amerika kaskazi,Afrika kaskazini ,Afrika magharibi na nchi za mashariki ya katinakusini magharibi mwa Asia.
Alisema Katika kipindi hicho Watanzaniay 6 waliokamatwa nchi za nje wakijihuisha na usafirishaji haramu wa kemikali bashirifu zaidi ya kilo 100 za Ephedrine, na Pseudoephedrine zinazotumika kutengeneza dawa za kutibu mafua na kikohozi na mwaka huu mamlaka imeteketezwa
Mwisho