“Ninatoa siku 7 watendaji wa vijiji kusanyeni hela mlizokubaliana kwa ajili ya kituo cha afya kwa kila kijiji”
Kamati ya fedha na mipango Halmashauri ya wilaya ya Monduli imefanya ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa kituo cha Sepeko.
“Hii hospitali haijengwi kwa faida ya mtoto wa kimai au mtoto wa Issack inajengwa kwa manufaa ya wananchi wa sepeko na nje ya sepeko, niwaelekeze watendaji wa vijiji natoa siku 7 wekeni mikakati ya kupata zile fedha mlizokubaliana kila kijiji kutoa million 10 mzilete hapa ujenzi uendeleee” issack
“Wakati wa harambee nilisema halmashauri kupitia mapato yake ya ndani itatoa millioni 50 na nitangaze hapa kwamba tarehe 15 mwezi huu fedha hizo zitaletwa hapa sio kwa ajili ya kulipa madeni ni kwa ajili ya kupaua na tutengeneze angalau vyumba vitatu ili tuweze kuhama kwenye lile jengo” .issack
Pia amewaomba wajumbe aliombana nao kuridhia kuelekeza fedha zitakazoelekezwa na serikali kwa upande wa afya kuipa kituo hicho cha sepeko Kipaombele ili kiweze kukamilika, na kuwataka watendaji wa vijiji na kata kuacha siasa kwenye maendeleo ya wananchi.
Akizungumza mwenyeji na Diwani wa kata hiyo Diwani Kimaai amewashukuru wananchi wa kata hiyo na wa vijiji kwa kuliibua swala hilo la ujenzi wa kituo cha afya ,Ofisi ya mbunge kwa kuwa mstari wa mbele katia uendeshaji wa harambee ilofanyika hivi karibu , na amekiri kuwepo kwa baadhi ya watendaji wazembe na wakaidi wa maendeleo.
” niwashukuru kamati ya fedha kwa kufika hapa tumejitahidi sana kwa nguvu zetu kama mnavyoona tumefikia Hatua ya kufunga lenta wadau wametoa material manake isingekuwa hivyo tusingefika hapa , watu waliahidi fedha nyingi na bado hazijakusanywa , nashukuru sana mwenyekiti kwa maelekezo yako hayo ya watendaji kukutana na Afisa utumishi mimi pia ni diwani kuna mtendaji wa kijiji cha lendikinya amekuwa mkaidi hasikiii ukimpa taarifa ya kikao hasikii naomba hata kama kesho akija ofisini kwako Afisa utumishi hata asiporudi aishie hukohuko hana msaada kwetu” alisema kimaai
Awali wakati akisoma taarifa juu ya utekelezaji wa mradi huo kaimu Afisa Maendeleo Kata ya sepeko bwana Beatus Mushi Amesema katika harambee iliyofanywa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha sepeko jumla kuu ilipatikana shiling millioni 248 ,zikiwemo millioni 50 Ahadi ya Halmashauri , Millioni 40 kutoka kwa vijiji 4 vinavyounda kata hiyo , na cash ni shilingi 3,996,100/=, Ambapo fedha ziliendelea kuchangwa kupitia account ya kamati ya harambee shilingi 15,065,100/= na baadaye account hiyo kwa makubaliano ya mkurugenzi na wataalamu waliamua kufufua account ya kata ilikuwa lala (Dormant) , na sasa Account hiyo imekusanya shiling 16,600,000/=
“Hadi sasa mradi huu umegharimu zaidi ya millioni sitini 60,056,000/=,
Vijiji vipo vinne na waliotoa mchango ni kama ifuatavyo mti mmoja 4.8 miliion, Arkaria 2.15 millioni , Lendikinya 0, na Arkatan 0.
Bwana Mushi ameongeza kwa kusema changamoto kubwa katika mradi huo ni kuwa na Account lala yaani dormant kipindi cha harambee hadi leo, watu waliohaidi kutotimiza ahadi zao , kuchelewa kwa kibali cha ukusanyaji wa michango kwa wananchi,pamoja na kushindwa kuwalipa Mzabuni.