Kesi dhidi ya sabaya kukatiwa rufaa na jamhuri imenguruma leo katika mahakama kuu kanda ya Arusha huku upande wa serikali wakieleza hoja zao saba mbele ya majaji watatu wa rufani
Kesi imesikilizwa kwa muda wa masaa saba ambapo pia mabishano ya kisheria kwa upande wa utetezi wa sabaya na serikali ulikua mkubwa ambapo majira ya saa kumi na moja kesi hiyo ilimalizika na huku majaji wakisema maamuzi ya rufani hiyo itatolewa baadae kupitia kwa msajili wa mahakama kutoa taharifa kwa mawakili wa pande zote mbili
Kesi ilikua ikisikilizwa na majaji watatu wakiongozwa na Mwenyekiti Jaji Jacobs Mwambegele, Jaji Ignas Kitusi na Jaji Leila Mgonya,