Na Mwandishi wa A24tv .
huyo wa Kijiji Pendeza anahisa asilimia 75 na Kijiji kinamiliki hisa asilimia 25 lakini shughuli zote za uendeshaji zinafanywa na Pendeza na uzalishaji ukipatikana kila mmoja anapaswa kupata haki yake kwa mujibu wa mkatana.
Alisema madini ya ruby yanayozalishwa yanapaswa kuwekwa mezani ili bodi ya usimamizi wa mgodi ya Kijiji ijue na kabla ya mgao na shughuli zote zisimamiwa na maofisa wa Wizara ya Madini kabla ya serikali kuchukua kodi yake.
Waziri Kiruswa aliwataka waendesha shughuli za uchimbaji kushirikiana na Bodi ya Kijiji yenye wajumbe tisa katika shughuli za kila siku na uzalishaji ukipatikana ili kuondoa malalamiko kwa baadhi ya viongozi na wananchi kwa ujumla.
Naye Diwani wa Kata ya Mundarara,Alaise Mushao kabla alidai kuwa Pendeza hatoi ushirikiano na uongozi wa Kijiji na amekuwa akichukua pesa za viroba kwa wananchi na anazalisha na kuuza madini ya ruby bila kushirikisha viongozi kama mkataba unavyosema .
Mwisho