Na Richard Mrusha
MBUNGE wa Jimbo la Kwela na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge na uwekezaji wa mitaji ya umma ,Deus Sangu Ameongoza kamati hiyo kwa kufanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali inayoendeshwa na Kampuni ya SUMAJKT ya uzalishaji Mali.
Amesema kipekee wamepata fursa ya kutembelea sehemu kuu mbili kwanza wametembelea Kampuni tanzu ya uzalishaji Kwa maana ya uzalishaji nguo pia kampuni tanzu nyingine ya uzalishaji Maji na kikubwa nikuendelea kuipongeza Serikali inayoongozwa na Rais DKT.Samia Suluhu Hassan kwanamna ambavyo ameiwezesha SUMAJKT katika uwekezaji .
Sangu ameyasema hayo Leo Novemba 15 mwaka huu jijini Dar es laam, ambapo Ambapo kamati hiyo imejionea kiwanda cha nguo ambacho kimewekeza fedha takribani milioni 361 na kwakweli kazi ni kubwa na Serikali inastahili pongezi na uzalishaji unaendelea hapo.
“Ni uzalishaji mkubwa na uwekezaji huu umeweza kuzalisha na Mwanzo ilikuwa na uwezo wa kuzalisha nguo 350 lakini uzalishaji wa aina mbili na nyingine imeongezeka na Sasa wanazalisha pisi 500 na bado wanahitaji kupewa nguvu zaidi na sapoti Ili waweze kuzalisha pisi 1000 Kwa siku na kwakweli tunaona Kwa namna walivyojipanga na namna ambavyo wanawateja wengi na wamefikia hatu ya kupata masoko hadi nje ya nchi .Amesema Mbunge Sangu.
Nakuongeza kuwa “tumeambiwa hapa wanawateja mpaka visiwa vya komolo kwahiyo uwekezaji huu kama kamati tuemeona niuwekezaji ambao unatia hamasa na unaleta tija si tu kwamba SUMAJKT wanafanya uzalishaji Kwa ajili yao peke yao bali pia wanatoa fursa ya ajira Kwa vijana wetu na tumeona vijana takribani 350 hapa wameajiliwa ambao wengine ni askari wa Jeshi la wananchi wengine wanatoka uraiani hivo asilimia 70 ni vijana kutoka uraiani .”Amesema
Amefafanua kuwa wao kama kamati ya kudumu ya Bunge ambao pia wanaangalia uwekezaji wa mitaji wataendelea kutoa sapoti kubwa Kwa taasisi ya SUMAJKT. ili uwekezaji zaidi uweze kuwekwa kwasababu wanaona shughuli zinazofanyika hapo zinatija kubwa kw uchumi wa nchi na uchumi wa mtu mmoja mmoja hata pale wanapotoa ajira Kwa vijana .
Pia wanaona uwekezaji uliofanyika wa takribani sh.bilioni 1.83 kwenye kiwanda cha uzalishaji Maji na uwekezaji huo umeweza kuleta tija kubwa wametoka kuzalisha chupa 3200 na Sasa chupa 10000 kwahiyo ni rai yao wao na wataendelea kuisimamia serikali kama kamati inasimamia uwekezaji wa mitaji waweze kuwawezesha SUMAJKT. Ili waweze kuzalisha Kwa wingi kwasababu soko ni kubwa na ukiona kiwanda cha Maji wanachozalisha uhitaji ni mkubwa zaidi ya uzalishaji wao kwahiyo wakiwezeshwa kupewa mtaji wa kununua mitambo zaidi watawezesha kufikia soko kubwa na kuongeza kipato na kitaongeza mchango na kukuza uchumi Kwa ujumla .
Mbunge ambaye ni Mwenyekiti wa kudumu ya Bunge ameongeza kuwa kama kamati Wana Rai ya aina mbili kwanza kutoa wito Kwa Taasisi za serikali hata za watu binafsi kwasababu soko la SUMAJKT. haliwalengi wenyewe tu hata watu binafsi wanafursa na milango Iko wazi na bidhaa zao zina ubora wa hali ya juu kwahiyo rai yetu kama kamati Ili waweze kuhakikisha Taasisi ikuwe zaidi na wachangamkie fursa hiyo ya kununua bidhaa za Maji ,nguo lakini pia wanazo bidhaa nyingi na hiyo nikutona na Taasisi yenyewe inaendeshwa Kwa ueledi zaidi na kinidhamu kubwa hivyo huduma wanazotoa Kwa wananchi zitakuwa na tija kubwa sana.
Ameongeza kuwa Kwa taasisi za serikali wanaendelea kutoa rai kama kamati ya Bunge kwamba wamekuwa na kawaida ya kuchukua huduma bila kulipa madeni na SUMAJKT. wanakabiliwa na changamoto hilo ya kuzidai Taasisi nyingi za serikali na kuwa na madeni hayo mengi yanaweza kuzolotesha kufanya mtaji kuzolota hivyo kama kamati ya Bunge wanaendelea kuhimiza Taasisi zote za serikali zinazodaiwa na SUMAJKT.waanze kurejesha fedha hizo ili kuiwezesha taasisi kusonga mbele.
Akizungumzia kuhusu kutanuka soko Mbunge Amesema kuwa kama Bunge wameendelea kuishauri Serikali lakini kumpongeza Rais Dkt.Samia na katika jambo kubwa ambalo amelifanya ni mahusiano ya kidiplomasia ya uchumi ambayo ndio fursa pekee kupitia Wizara ya mambo ya nje wamekuwa wakifanya makubaliano mbalimbali kuwatangazia fursa za kiuchumi zilizopo ndani ya nchi hivyo pongezi Kwake Rais Dkt Samia.
Kwa upande wake mkuu wa JKT na Afisa mtendaji Mkuu wa SUMAJKT. Meja jenerali Rajabu Mabele
Anaishukuru kamati ya kudumu ya Bunge ya uwekezaji na mitaji ya umma kwanamna ambavyo wanaendelea kutuelekeza na kuhakikisha kwamba tunafanya vizuri zaidi ,maboresho wanayoyaona ya kiwanda hicho kimeboreshwa na kama alivyosema Mwenyekiti tumetumia zaidi ya milioni 300 kuhakikisha kwamba tunaboresha zaidi ikiwemo kuongeza mashine.
Nakwamba kulikuwa na laini mbili za uzalishaji lakini sasahivi tunalaini sita na uzalishaji wa kuzalisha nguo 300 Kwa siku hivi Sasa tunazalisha nguo 700 na lengo letu nikuelekea katika kuzalisha nguo 1000 Kwa siku kwahiyo bado tunaendelea kuzalisha na masoko kiukweli tunamshukuru sana Rais DKT. Samia kwakuendelea kutanua wigo katika diplomasia ya uchumi kwani mahusiano na nchi nyingi ni mazuri sana napia hata viongozi wa majeshi wanapotembela Tanzania na Jeshi la Ulinzi Tanzanaia wamekuwa wakitembelea kiwanda hicho na Viwanda vingine vya SUMAJKT .Amesema Meja jenerali Rajabu Mabele.
Mwisho .