Na Mwandishi wa A24tv
Mkuu wa Wilaya Siha mkoani Kilimanjaro Christopher Timbuka,amewapa kongole jumhiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT),Wilayani humo kwa kuweza kusaidia kutatua migogoro mbali mbali iliyopo kwenye jamii jambo ambalo linachangia kuleta maendeleao
Haya yamesemwa wakati wa maazimisho ya siku ya Maridhiano ambapo kiwilaya imefanyika Hospitali ya Wilaya kwa kufanya usafi , kutembea wagonjwa na kuwalia hali sambamba na kuchangia damu sala.
Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, amesema Jumuhiya hiyo imesaidia kutatua migogo mbali mbali ikiwamo ya migogo ya Aridhi pamoja na kutoa ushauri
“Ni kweli migogoro midogo midogo na mingine ya inayokuzwa inakuwa ni mingi lakini mnatusaidia sana kuhakikisha kwamba mnaituliza na kuwa na Amani ni jambo jema”amesema Timbuka
Mimi mwenyewe shahidi kwamba nimekuwa nikiwaagiza katika baadhi ya maeneo mwende mkanisaidie ili kuweka mazingira vizuri na mmekuwa mkienda matokeo tunayaona,
kweli tunawapongeza sana kwa hilo,tunawashukuru sana kwa moyo mnatuonyesha wa kutatua migogoro ili kuleta maendeleao kwa Wananchi wa Siha na Tanzanian kwa ujumla
“Wote tunafahamu sehemu yenye migogo maendeleao kuwepo maeneo haya hakuna ni jambo lisilowezekana,niwapongenze tuendelee kushirikiana tufikie malengo tulilokusudia”amesema Timbuka
Pia tunawapongeza kwa kuitembelea wagonjwa na kuwajulia hali na hatimae kuwasaidia kwenye suala la uchangiaji wa Damu salama,kama vilivyosema sadaka ya damu ni sadaka ya kipekee haina mbadala
Awali Mwenyekiti wa Jumuhiya hiyo, Gerard Mollel amesema katika kuadhimisha siku ya Maridhiano kiwilaya wamefanya usafi ,kutembele wagonjwa pamoja na kujitolea damu salama
Ambapo amesema maadhimisho haya kitaifa yatafanyika mkoani mbeya March 6 mwaka huu na kwamba jumhiya hiyo inashughulika na kutatua migogoro mbali mbali kwenye jamii ya na pia kuibua iliyofichikani ili kuwa na amani
Matias Sabiku mratibu huduma za maabara ngazi ya Wilaya pia mratibu wa upatikajj wa Damu salama katika halmshauri hii,
Amesema halmshauri wanahitaji Damu salama ambapo kimuongozo Kitaifa wamepewa kukusanya chupa 882 kwa mwaka ambao ni sawa na chupa 72 kwa mwezi hayo ni mahitaji kwa halmshauri hii ,
Ambapo zitatumika Hospitali ya Wilaya, Hospitali ya Taifa ya kibongoto na pia kuna vituo vya Afya.
Mwisho
Mwisho