Na GEOFREY STEPHEN ARUSHA .
Wanafunzi katika Kata ya Ngarenaro Jijini Arusha wametakiwa kutokaa kimya dhidi ya vitendo vya Ukatili wa kijinsia pindi vinapotokea au kuona viashiria vyake na badala yake watoe taarifa kwenye ofisi za serikali ama kituo chochote cha Polisi.
Wito huo umetolewa leo Februari 02, 2024 na Mkaguzi Kata ya Ngarenaro Jijini Arusha, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Tadey Tarimo wakati akitoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia katika shule ya Msingi Swift Juniour Academy School iliyopo mtaa wa kambi ya fisi katika kata hiyo.
A/INSP Tarimo amewatoa hofu wanafunzi hao na kuweleza kuwa, Polisi siyo adui bali ni watu wema kwao na hivyo wasiogope kutoa taarifa za vitendo vya ukatili au viashiria vya uhalifu.
Pia Mkaguzi huyo ameendelea kuwaeleza kuwa wasiogope vitisho vinavyotolewa na watu wanaowafanyia vitendo vya ukatili kwani serikali kupitia Jeshi la polisi lipo kwa ajili kuwalinda ili kufikia ndoto zao
Mwisho amewataka wanafunzi hao kuwaheshimu wazazi, walezi pamoja na walimu lakini pia kuzingatia masomo ili waweze kufikia malengo yao kitaaluma na maisha kwa ujumla.
Mwisho .