Na Mwandishi wa A24Tv .
Kwa ufupi SMAUJATA mkoani Kilimanjaro weweka mkakati wa mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili ikiwamo ubakaji na ulawiti vinavyozidi kuongeza
Moshi,Viongozi wa Taasisi huru ya Shujaa wa maendeleao na Ustawi wa jamii Tanzanian (SMAUJATA) mkoani Kilimanjaro wameweka mkakati wa kuendelea na mapambana dhidi ya vitendo vya ukatili ikiwa ni pamoja na ulawiti na ubakaji ambavyo vimekuwa vikiongezaka kwa kutoa elimu sehemu mbali mbali ikiwamo shuleni ,vyuoni ,sokoni na pia kuanzisha vilabu mashuleni vya kupinga ukatili huo.
Haya yamejiri katika kikao cha mpango kazi 2024 na 2025 ya kujiwekea mpango mkakati kwa ajili ya kuendelea na mapambano dhidi ya matendo hayo katika mkoa huu
Stella Mashinda katibu wa (SMAUJATA), mkoani Kilimanjaro, Akizungumza na viongozi wa ngazi zote mkoani hapa katika kikao kilichofanyika katika jengo la Uchumi Moshi mjini, amesema wamejiwekea mkakati wa mapambano dhidi matendo hayo ikiwa ni pamoja na kujikita zaidi katika kutoa elimu hasa kwa watoto kwani ndiyo waathirika wakubwa.
“Ni kweli tumejiwekea mpango mkakati kwa ajili ya kuendelea na mapambano ya ukatili katika mkoa wetu tukijikita katika kutoa elimu kwani elimu inampa mtu mwanga wa namna ya kukabiliana na kujikinga dhidi ya matendo hayo, kwani kinga ni bora kuliko tiba amesema Stella ,
Stella amesema kwa mikakati hiyo waliojiwekea kwa kushirikiana na wadau wengine wakupinga vitendo hivyo ikiwamo Ustawi wa jamii matendo hayo yanaweza kupungua au kumalizika kabisa na mkoa kubaki salama , kunzia mwezi April hadi June itakapofika siku ya mtoto wa Africa tuwe tumeweza kuendelea na mapambano tufahamu tumefikia kiwango gani.
Staki lymo Mwenyekiti kamati ya ufutiliaji vitendo vya ukatili mkoani hapa, amesema vitendo vya ukatili vinazidi kuongeza siku hadi siku,kutokana na hilo na kikao hiki tumedhamiria kufanya kazi kwa nguvu kama walivyosema viongozi waliotangulia
Kwa upande wake Yunisi Nonga katibu wa SMAUJATA Wilaya Siha Mkoani hapa, amesema ushiriano kwa baadhi ya watu katika ofisi umekuwa mdogo hivyo wakati mwingine kurudisha juhudi za kupambana na maswala hayo kurudi nyuma.
Amesema kwa sababu viongozi wamesikia na hizo changamoto wameahidi kuzifutilia nimatumaini yake lengo la mapambano hayo yatasonga mbele katika mkoa huuu,
” Ni kweli kama ushiriano utakuwepo vizuri matukio haya yatapungua,kaulimbio ya SMAUJATA kata Ukatili wewe ni “amesema Nonga.
Mwisho.
Mwisho