Na Geofrey Stephen Arusha
Anae zungumza na vyombo vya habari ni Mkurugenzi wa Kilifair ambaye pia ni mwandaaji wa maonyesho hayo ,Dominic Shoo
Meneja Mkuu kutoka hoteli ya Serena Daniel Sambai akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maonyesho hayo mkoani Arusha.
Atusha .Waziri wa Maliasili na Utalii Angellah Kairuki anatarajiwa kuwa mgenirasmi kwenye ufunguzi wa maonyesho ya kimataifa ya Karibu -Kilifair 2024 yanayotarajiwa kufanyika Juni 7 hadi 9 mwaka huu mkoani Arusha .
Aidha katika maonyesho hayo wanunuzi zaidi ya 600 wa Utalii kutoka nchi 40 duniani na waonyeshaji pamoja na wadau 468 wa utalii kutoka nchi 37, wamethibitisha kushiriki maonyesho ya kimataifa ya Karibu -Kilifair yanayotarajia kuanza Juni 7 hadi 9 mwaka huu jijini Arusha.
Vile vile wadau hao na wanunuzi wa utalii watatembelea vivutio vya utalii, ili wakawe mabalozi wazuri kwenye nchi zao.
Akizungumza mkoani Arusha Mkurugenzi wa Kilifair Ltd ambao ndio waandaaji wa maonyesho hayo ,Dominic Shoo amesema lengo la maonyesho hayo ni kutangaza vivutio vilivyopo nchini na wakauze nchini kwao.
“Siku hizi tatu tunatarajia kuwa na kiwango kikubwa cha biashra kwa sababu lengo letu kubwa kukutanisha wadau toka mataifa mbalimbali duniani, kuja kujua vivutio vyetu hapa Tanzania, wavitembelee na kuweza kuwa mabalozi wazuri, kwa ajili ya kuuza vivutio vya Tanzania,”amesema.
Amesema mwaka huu onyesho hilo ni kubwa kuliko la mwaka jana, sababu wamekuwa na waonyeshaji zaidi na mwamko wa wanunuzi ni mkubwa kuliko mwaka jana na wamekua na kiwango cha juu, kuliko mwaka jana kutokana na vitu ambavyo wameweza kuvinunua, ili kuhakikisha onyesho hilo linalingana na hadhi ya viwango vya kimataifa.
Amesema kuwa Juni 8 watakuwa na tamasha la muziki, utakaoleta watu pamoja na utakuwa wa kiwango cha kimataifa kutokana na kushirikisha wataalamu wa burudani.
“Kwa sababu siku hizi tatu tumeona tutakuwa na wageni wengi Arusha, lakini hawana burudani ya kutosha tukaona kuliko wakapate burudani sehemu tofauti, ambazo hazina hadhi tumeamua kuwaandalia kitu kipya kitakachowapa burudani Juni nane mwaka huu,hapa hapa viwanja vya Magereza na tumeunga na wataalamu wa burudani tunashirikiana nao,”amesema Shoo.
Hata hivyo amesema utalii unakua, ambapo msimu huu wa utalii umefunguka mapema ukilinganisha na mwaka jana, ina maana huhitaji wa kiu ya kwenda kwenye hifadhi ni mkubwa.
“Lakini watu wana hoteli mpya nyingi na wanabishara mpya, wanataka juhakikisha wengi wanazijua na kupitia hapo wajue taarifa zao na bei zake,”alisema
Shoo ameongeza kuwa, maisha sasa hivi ni Afrika, ukienda nje ya nchi onyesho lolote linalokosa Mtanzania wanashtuka, sababu Afrika nkombozi wao Tanzania kwenye sekta ya utalii.
Ameyataja baadhi ya mataifa hayo yafakayoshiriki knyesho hilo, kati ya 40 wanakotoka wanunuzi wa utalii kuwa ni Ujerumani, Amerika, Italia, nchi za Afrika Mashariki, Aftika Kusini na Asia.
Meneja Mkuu kutoka hoteli ya Serena Daniel Sambai amesema kuwa, kila mwaka ongezeko la wanunuzi limekuwa likiongezeka kutoka nchi 34-40 na hii ni kutokana na uongozi na usimamizi imara wa waandaji hao ambao umekuwa mkubwa .
“Naupongeza uongozi wa Karibu Kili fair kila mwaka wanunuzi wanaongezeka na cha msingi nisema tuu wakija wanunuzi Wazuri wanachangia kuleta wageni wengi Nchini na nchi zimeendelea kuongezeka.”amesema Sambai.
Naye Mkuu wa kitengo cha masoko na mauzo kutoka kampuni ya Media works Noel Petro ,amesema asiilimia 70 ya wateja wao wanatokana na utalii na ndiyo maonyesho ya kipekee sana huku akiiomba serikali kujengwa kwa mabanda ya maonyesho ya kudumu ili kuwepo kwa mazingira salama nyakati zote.
“maonyesho haya ni ya kipekee kwetu sisi kwani yanaleta fursa ya utalii kwani wateja wetu wakubwa wanatokana na utalii,kila mtu atakayekuja kwenye banda lao atapata punguzo kubwa la gharama na wamekuja na fursa ya kupunguza changamoto ya taka ngumu ikiwemo chupa za maji ili kuokoa mazingira”amesema
Mwisho.