Na Mwandishi wa A24tv Siha,
Mwanafunzi wa Darasa la saba shule ya Msingi Majengo nyati Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro ,Ebeneza Msuya (14),amelazwa katika Hospitali ya rufaa ya KCMC ,akisubiri kuongezewa damu ili kufanyiwa uchunguzi baada ya kupigwa na mwanafunzi mwenzake na kumsababishia kutoka dama sehemu za siri
Pia ameomba wasamaria weme kujitokeza ili kumchangia damu ilikufanikisha zoezo la kufanya uchunguzi liwezekufanyika ,Tukio hilo limetokea may 13 mwaka huu katika shule hiyo ambapo chanzo cha ugomvi inadaiwa baada ya kuchanwa namba ya mtihani wake moku na alipohoji ndipo ugomvi ulipo zuka
Angela Nyoni mama mzazi wa mwanafunzi huyo Akizungumza na mwananchi Digital kwa njia ya simu, Amesema kinachosubiriwa kwa sasa ni kuongezewa damu ili zoezi lingine liendee lakuangalia Afya yake liweze kuendelea ,amepigwa sehemu za tumboni na damu nyingi zinatoka kwenye njia ya haja dogo
“Ni kweli toka may 13 mwaka huu tulipofika hospitali alitakuwa kufanyiwa uchunguzi sehemu mbali mbali za mwili wake lakini anaupungufu wa damu na sehemu ya kupata damu ni tatizo ,Madaktari wananiambia nisubiri hadi damu itakapopatikana wananishumbua wananiambia sasa tunafanyaje kama damu hakuna”Amesema Angela
Angela may 13 mwaka huu mtoto wake alitoka shuleni majira ya jioni na kumpa taarifa kwamba amepigwa na mwanafunzi mwenzake wanayesoma naye darasa moja na kwamba sababu ya ugomvi ni mwanafunzi huyo kuchana namba ya mitihani na alipohoji ndiyo ugomvi ukatokea ,alimpiga mateke sehemu ya tumboni damu zikawa zinamtoka sehemu ya Siri
Baada ya hapo walimpeleka Hospitali ya Wilaya hiyo na baadaye kumuamishia hospitali ya KCMC Moshi na kutakiwa kuongezewa Damu ili zoez la uchunguzi liwezekufanyika hadi leo hatujapata damu ,nimewataarifu ndugu Wamesema watakuja
Hivyo nawaomba wadau mbali mbali ,Mbunge wa Siha Godwin Mollel pamoja na wasamaria mwema kujikeza ili wawaze kumsaidia mtoto aweze kupata matibabu na kurejea nyumbani na kuendelea na masomo
Mwenyekiti wa kitongoji cha Majengo Robart Ullotu ,Amesema hizi taarifa amezipata ,kwa sasa yupo mtoto yupo Hospitali ya rufaa ya KCMC Moshi,hakuna kinachoendee Madaktari wanasubiri kumuongezea dama ili kumfanyia operesheni ,leo ni karibu siku ya sita bado hatujapata matibabu ni hatari sana
Robart anasema amempigia mama mzazi wa mwanafunzi huyo amem fahamisha kwamba mgonjwa anahitajika kuongezewa damu ,lakini haijapatikana
Labda nijaribu kuwasiliana na Ndugu zake ni familia masikini haijiwezi,tujue tunafanyanini
Peter Msaka afisa Ustawi wa jamii Wilayani humo,Amesema mtoto huyo wanataarifa naye na yupo Hospitali ya KCMC na kwamba mtoto aliyeusika tukio hilo anashikikiwa na jeshi la Polisi kituo cha polisi Sanya juu
Mwisho