Na Bahati Hai .
Mahakama Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro imemuhukumi Mkazi wa Wilaya ya Longido Mkoani Arusha kwenda jela maisha kwa kosa la kubaka mtoto wa miaka( 8) wa kike.
Siha, Mkazi wa Wilaya ya Longido Mkoani Arusha cha Samweli Mayani (29),mkulima amehukumiwa kwenda kutumikia kifungo cha Maisha jela kwa kosa la kubaka mtoto wa miaka 8 Mkazi wa Kijiji cha Embokoi Wilayani siha
Mshitakiwa huyo alifika katika Kijiji hicho kwa lengo la kufanya kazi za vibarua cha kulima
Mwendesha mashitaka wa Serikali David Chisimba mbele ya Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mahakama hiyo Jasmine Abdul amesema tukio hilo lilitokea November mwaka jana
Mwendesha mashitaka huyo ameeleza kuwa mshitakiwa akiwa anaendelea na shughuli hizo za kufanya kibarua ,alimuona mtoto huyo akitoka shuleni na alipofika nyumbani mshitakiwa alimfuata na kumkuta mtoto huyo yupo peke yake ,ndipo apomlaghai kumwambia mama yake anamuita
Baada ya mtoto huyo kutii wito aliondoka na mshitakiwa na walipofika mbele kidogo kulikuwa na kichaka ndipo jamaa aliponyia kitendo hicho cha ukatili na kumsababishia maumivu
Baada ya kitendo hicho alimtishia kwamba asiende kusema,hata hivyo mama mzazi alimgundua kwamba mtoto wake hayapo katika hali ya kawaida kutokana kwa kushindwa kutembea vizuri na hali kuwa mbaya
“Ni kweli alimdanganya mtoto kwamba anaitwa na mama yake mzazi mtoto bila kujua thumuni la huyo jamaa alimfuata ndipo alipotimiza matakwa yake uku akifahamu fika kufanya hivyo ni kosa”amesema Chisimba
Chisimba amesema kitendo alichofanya ni kinyume na kifungu namba 130 (1)(2)(e)na 131(2)cha Sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16 Kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022,ambapo kesi hiyo ilikuwa na mashahidi 4 akiwamo Daktar na muhanga mwenyewe
Kabla ya kutolewa hukumu hiyo Hakimu ,alimtaka mshitakiwa kujitetea ambapo aliomba Mahakama kumuonea huruma kwa kuwa ana wake wawili na watoto hivyo wanamtegemea ,case 38567 ya mwaka 2024
Hata hivyo Hakimu ilisema kutokana na kusa hilo kutokuwa na mbadala wa adhabu zaidi ya kifungo kutokana na umri wa muhanga kuwa miaka 8
Na pia kukithiri kwa vitendo hivyo ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hivyo mahakama inakuhukumu kwenda jela kutumikia kifungo cha maisha jela
“Ni kweli vitendo vya ubakaji na ulawiti vinazidi kuongeza ndani ya Wilaya yetu ili iwefundisho kwa wengine unakwenda kutumikia kifungo cha Maisha jela”amesema Jasmine
Mwisho