Siha,
Wilayani siha mkoani Kilimanjaro imekusudia kuitaitisha kikao maalumu cha kujadili changamoto mbali mbali zinazosababisha ufaulu mbaya kwa wanafunzi katika Wilaya humo
Kauli hiyo imetolewa wakati wa uzinduzi wa kitabu cha kuwajengea uwezo mwanafunzi ili aweze kufanya vizuri kwenye masomo yake iliyoganyika katika ukumbi wa Rc, Sanya juu Wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya hiyo Christopher Timbuka Akizungumza Mara baada ya kuzindua kitabu hicho na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwamo wa Serikali , Chama na Dini ,amesema kikao hicho ni muhimu kwa mstakibali wa elimu Wilayani humo
“Ni kweli nampongeza kwa jambo hili ametuwahi na sisi tumedhamiria kusitisha kikao maalumu kujadili kwanini ufaulu uharizishi kwenye Wilaya yetu wa wadau wa elimu ikiwa ni pamoja na Maafisa elimu na wakuu wa shule watahudhuria”amesema Timbuka.
Timbuka amesema,ameongea na Mkurungenzi mtendaji wa Halmshauri ni kufanya tathimini ya sababu ya sababu hasa inasababisha ufaulu hauridhishi kwenye Wilaya , Wanafunzi wa kidato cha nne wanaofanya mtihani asilimia 70 hawafanyi vizuri inamaana asilimia 30 ndiyo wanafanya vizuri hii sio sawa
Kwa hiyo tunataka kufanya kikao cha tathimini na tumeshapanga kikao hicho, watakuwa wadau wa elimu ,wakuu wa shule,walimu wakuu Maafisa elimu , Mkurungenzi mtendaji wa Halmshauri na wale wote wanaousika
Kwa upande wake Mkurungenzi mtendaji wa Halmshauri hiyo Haji Mnasi ,amesema atahakikisha kitabu hicho kinafika sehemu mbali mbali kwe lengo la kusomwa
Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi (CCM), Wilayani humo Emanuel Mushali,ametoa pongenzi kwa mwandishi huyo na kwamba hii ni sera ya chama na kumuunga mkono Rais Samia Suluhuu Hassani kuhakikisaha elimu kwa watanzania wote.
Pia amempa kongole mwandishi huyo kwamba mauzo ya awali nakala 500 ya kitabu hicho yatakwenda kusaidia umaliziaji wa ujenzi wa Kanisa TAG lilipo Sabuko Wilayani humo
Awali mwandishi wa kitabu hiki mfanyakazi kutoka shirika Compassion International Tanzania Audats Kisato , amesema sababu ni kuongeza ufaulu kwenye shule za binafsi na za serikali
,
kuwasaidia watoto wajue mbinu za kujifunza,
Kusaidia wamiliki wa shule namna ya Kuwasaidia wanafunzi kufaulu na kuelewa.
Na kusaidie wazazi mbinu za Kuwasaidia watoto namna ya kuelewa na kufaulu masomo
Kwasiadia wanafunzi wenye uzito wa kuelewa
Mwisho