Na Mwandishi wa A24tv.
Wananchi wa Kijiji cha Ormelili Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro wameombwa Serikali kuingilia kati ili apatikane mwanafunzi wa kidato cha pili (Naishie Mollel)anayesoma shule ya Sekondari Ormelili anayedaiwa kuchukuliwa na vijana wanne wa jamii ya kifugaji wa Kijiji hicho na kutoweka kusikojulikana
Mwanafunzi huyo inadaiwa alichuliwa na vijana hao junuari mwaka baada ya kufungua shule alipokwenda Kanisani na wenzeke kunya usafi na taarifa kutolewa kwenye vyombo usika lakini hadi leo hajapatikana.
Wananchi hao wakiongea na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti,wameomba Serikali Wilayani humo kuingilia kati ili aweze kupatikana kwa mwanafunzi huyo ina kuendelea naasomo
“Ni kweli tunaomba Serikali kuingilia kati ili aweze kupatikana ,kwa sasa ni takribani miezi 4 haijulikani alipo wamesema” Wananchi hao
Joseph Laizer mmoja ya Wananchi hao amesema siku ya tukio mwanafunzi huyoa akiwa na mwenzake walikwenda Kanisa lilipo kijijini hapo kwa ajili ya usafi na kuimba kwaya ,wakati wanarejea nyumbani ndiyo wakakutana na vijana hao na kumchukua na kutoweka kusikojulikana
Amesema baada ya hapo mwanafunzi aliyekuwa anafuatana naye alikwenda kutoa taarifa kituo kidogo cha Polisi kilichopo kituo cha mabasi cha KIA Wilayani humo la kuchukuliwa maelezo
Laizer,amesema Wazazi wa pande zote mbili wapo hapo Kijiji ni kwanini wasibanwa ili wasema sehemu alipo mtoto huyo ,kwa sababu zipo taarifa kwamba ameozeshwa uko Maeneo ya Mkoa wa Tanga ,Serikali ifuatilie ili aweze kupatikana
“Ni kweli Wazazi wa pande zote mbili wa vijana hao wapo kijijini hapa ,vyombo usika vikiwamo Ustawi wa Jamii na Dawati la njinsia na watoto vikiwabana watasema alipo huyo mtoto”amesema Laizer
Pia ameomba Viongozi wa Wilaya kufanya ziara za Mara kwa mara katika shule za Msingi na Sekondari za Jamii hiyo na kufanya ukaguzi kujua kila darasa linawanafunzi wangapi hii itasaidia sana kuendelea kuwalinda watoto
Anna Molle anasema tabia ya kuozesha wanafunzi katika Maeneo ya Jamii hiyo hasa kwenye kata za Donyomurwa ,Oromelii,Orkolili , Karansi, Gararagua, ni kitu cha kawaida na wanafichiana siri na ukibaini kutoa wanaanza kukutenga na kuanza kutishiwa maisha,
Hivyo tunaomba Serikali iangalie hili kwa jicho la tatu,watoto wakiume wao uachishwa shule na kwenda kuchunga mifugo
Mwenyekiti wa kiji cha Ormelili Jeremia Leizer amesema kwamba mtoto hajapatikana ,ili jambo Wazazi waliitwa shulenj na pia lilifika kituo cha polisi Sanya juu,sijajua limefikia wapi,leo tunakaa na Serikali ya Kijiji
Mwisho