Na Mwandishi wa A24tv .
Siha,Jeshi la Polisi Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro,linafanya operesheni ilikukamata wezi wanavunja na kuiba mali mbali mbali za Wananchi zikiwamo pikipiki,tv Radio jambo ambalo linarusisha juhudi za maendeleao nyuma
Kutokana na zoezi hilo kuendelea Wananchi Wilayani humo wameipongeza Jeshi hilo kwani wameweza kufakiwa kupata baadhi ya mali zilizoibiwa pamoja na wannunuzi wa mali hizo za wezi.
Mkuu wa Jeshi hilo Wilayani humo Zakia Shuma,kizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake,amesema zoezi hilo ni endelevu hadi uhalifu upungue na kuomba ushirikiano kwa Wananchi
“Ni kweli tumeanza zoezi la kuwasaka wahalifu wakiwemo wezi wa mali za watu mbali mbali tumefanikiwa kuwakama baadhi yao na wanaopokea Mali hizo za wizi “amesema Zakia
Zakia amesema kumekuwa na matukio mbali mbali ya wizi na uvunjaji ambao tumepokea katika kituo chetu kutoka sehemu mbali mbali ya wilaya yetu
Sasa kidogo ni swala ambalo kwa upande wetu hatukuona kwamba ni swala nzuri linajirudia ina maana wanapofanya tunao miongoni mwetu
Baada ya kuona vile tukasema sasa tuanze kazi ,tumefanya operesheni tuweze kuwabaini wanaousika na haya maswala
Tumeweza kufanikiwa ,tumefanikiwa kujua wanao iba wezi wetu,tumegundua na wale wanaopokea ndiyo imeturahishia sana
,ukimpata mwizi anayevunja na kuiba ,ukampata na yule anayechukua anayepelekewa hizo mali za wizi inakuwa ni raisi kupata kundi zima wanaoshughulika wanaofanya hizi shughuli
Amesema bado wanaendelea na operesheni,tumewza kufanya hapa SanyaJuu, tunaendea na sehemu nyingine tunataka kupunguza
Pamoja na zoezi hilo kuendelea lakini amewashauri Wananchi kwamba usalama unaanza na weo mwenyewe,niwashuruku kwa ushirikiano wao wanaotupa na waendelee kutupa ushirikiano huo
Jumanne Omari,katibu wa Jumuhiya ya maridhiano na Amani Tanzania kata ya Sanya juu, niwapongenze Jeshi la Polisi kwa kazi nzuri waliyoifanya,kwa kurudisha mali zilizokuwa zimeibiwa katika zoezi lenu ambapo mmefanikiwa kupata vitu vingi.
Omari Yusuph Mkazi wa Sanya juu amesema aibiwa ameibiwa charahani pamoja na tv na radio nashukuru kupitia Jeshi la Polisi amefanikiwa kupata charahani hiyo peke yake
” Jeshi la Polisi wametoa tangazo kwa wale walioibiwa vitu vyao wafike kituo cha polisi kuja kutambua mali zao nilipofika nifanikiwa kupata mashine ya kushonea lakini radio na tv sijapata matumaini kwa sababu wanaendelea na operesheni naweze kuja kupata vitu vilivyosalia nawashukuru “amesema Omar
Mwisho