Na Mwandishi wa A24tv -MANYARA
Watu watatu wamefariki Dunia na wengine watano kujeruhiwa kufuatia ajali iliyohusisha magari Matano pamoja na pikipiki Moja katika eneo la Mogitu Hanang Mkoani Manyara.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara SACP George Katabazi amesema waolifariki katika ajali hiyo ni Mwanamke aliyekuwa katika gari ndogo aina pamoja na Wanaume wawili waliokwenda kushuhudia ajali hiyo.
“Ajali imetokea usiku wa kuamkia leo katika mteremko wa Mogitu Hanang ambapo kulitokea ajali ya gari aina ya Scania mbili kugongana na kusababisha kuziba barabara na kufanya magari mengine kushindwa kupita kwenye barabara hiyo, Polisi walifika kwa wakati eneo la tukio ili kuruhusu magari kuendelea kupita”
“Wakati Polisi wakiruhusu magari kuendelea kupita kwa utaratibu ndipo kukatokea bus la kampuni ya Arusha Express likiwa linatokea Kagera kuelekea Arusha Dereva hakuchukua tahadhari na kushindwa kumudu gari hilo na kupelekea kugonga Scania moja kwa nyuma na kupoteza uelekeo na kupelekea kugonga pikipiki pamoja na gari ndogo aina ya Toyota Mistubish ikiwa ime-park pembeni kusubiria kupita baada ya ajali ya kwanza ambapo hii imesababisha Mtu mmoja kufariki papohapo”
“Baadaye bus hilo likagonga bus jingine ambalo nalo lilikuwa lime-park pembeni huku vifo vingine viwili ambapo wote Wanaume vikiwa vimesababishwa na kupitiwa na gari hilo wakati wakishuhudia ajali ile ya kwanza iliyotokea ya magari mawili aina ya Scania, kwa sasa magari hayo yameshaondolewa kwenye barabara kuu na shughuli za usafirisha zinaendelea kama kawaida”
Ends….