Na Bahati Hai
Jamii Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro imepewa angalizo kwamba Mtu anapokuwa na msongo unaochangiwa na changamoto za maisha suluhisho sio kukimbilia kunywa sumu,
Anaweza kuonana na mtu anayemuamini wakiwamo Wataalamu kutoka idara ya maendeleao ya Jamii na Ustawi Jamii waliopo Wilayani humo ili waweze kukaa na kushirikiana jambo hilo ili liweze kupatiwa ufumbuzi.
Haya yamejiri baada ya kuonekana swala kunywa sumu kwa baadhi ya watu kwa Wilaya hii limekuwa changamoto sana
Marck Masue afisa maendeleao ya Jamii Wilayani humo, Akizungumza na mwananchi Digital kwa njia ya simu ,Amesema hili swala watu kunywa sumu limekuwa changamoto sana kwenye Wilaya hiyo
“Ni kweli limekuwa changamoto kubwa , jambo amepata mtu ameashindwa kulibeba ameshindwa kumshirikisha mtu anaamua kunywa sumu hili limekuwa tatizo sana
Masue amesema hatua hiyo sio sahihi hata kidogo ,wapo wataalamu kwa ajili ya kazi hizo ,wakushauri na kuongea nao taratibu na baadaye kumtoa kwenye changamoto alizopata
Amesema swala hilo kwa Wilaya limekuwa changamoto sana ,Kunywa sumu maana yake Serikali inakushitaki maana unapunguza nguvu kazi ya Taifa,Hivyo ameishauri Jamii ijiepushe kukaa peke yao wanapopata matatizo ,
Kama nilivyosema awali tafute watu au mtu unayemuamini kaa naye mueleze changamoto zinazokusibu hii itasaidia kutatua tatizo kuliko kufikiri peke yake ambapo utashindwa kupata majibu na mwisho kuamua kunywa sumu akijua ndiyo suluhisho kumbe ni kuongeza matatizo
Mtu anakunya sumu kwa jambo ndogo tuu ambalo angekaa na watu wangemshauri namna ya kutatua tatizo
Idrisa Mndeme makamu Mwenyekiti wa Jumuhiya ya Maridhiano na Amani Tanzania Wilaya ya Siha (JMAT),amesema migogo inapotokea kwenye familia sehemu ya kukimbia ni kwa wazee wa ukoo pamoja na Viongozi wa Dini ili kusuluhisha tatizo badala ya kujichulia sheria mkononi ya kunywa sumu
Amesema June 9 mwaka huu alifika Hospitali ya Wilaya hii kwenda kuangalia wagonjwa ambapo alikuta wanaume wawili wamelazwa kwa madai ya kunywa sumu aina ya Gramason ,na kwamba kuna wengine walikunywa sumu wameruhusiwa kuondoka baada ya kupata matibabu hili ni tatizo
Mndeme amesema Mtu anapothubutu kujitoa uhai ni kosa kisheria,wanapotibiwa na kupona washitakiwe kwa mujibu wa Sheria,adhabu zitakazotolewa itakuwa funzo hata kwa wale wengine wenye mawazo kama hayo
Tusipo fanya hivyo tunaijengea jamii hasa watoto wetu wanaokuwa wanaona vitendo vile vya kunywa sumu ndiyo njia sahihi ya kumaliza matatizo
Jonh Philipo Mkazi wa Sanya juu ,ameombo maendeleao ya Jamii pamoja na Ustawi kutokana na changamoto za kimaisha zilivyo kwa Sasa ambazo zinasababisha msongo wa mawazo wajikite kutoa elimu sehemu mbali
“Ni kweli wakijita kutoa elimu inaweza kusaidia mtu labda alikuwa ana matatizo hayo ya usongo wa mawaza lakini kupitia elimu atakayopata itasaidia kubadili mtazamo”amesema Jonh
Mwisho