Na Bahati Siha .
Mkuu wa Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro , Christopher Timbuka,amewataka wadau wa maendeleo Wilayani humo kuhudhuria kikao maalumu cha kamati ya maendeleao Wilaya (DCC)kwa ajili ya ukusanyaji wa maoni ya Dira ya Taifa ya maendeleao 2050
Kikao hicho kitakaoshirikisha wadau mbalimbali wa maendeleao wakiwamo taasisi za Dini ,vyama vya Siasa na wawakilishi wa makundi yote muhimu katika jamii pamoja na mtu mmja mmoja wanakaribishwa kitakachofanyika ukumbi wa halmshauri hiyo
Haya yamesemwa leo na Mkuu wa Wilaya Christopher Timbuka, Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ,ambapo amesema lengo la mukusanyiko huu ni kupata maoni ya wadau wote waliopo Wilayani humo
“Ni kweli lengo kubwa la mukusanyiko huu ni kupata maoni ya wadau wote Wilayani humu Dira ya 2025 hadi 2050 ni muelekeo ambao Serikali inataka kufanya katika kufikia maendeleao ya Wananchi wa nch hii “esema Timbuka
Timbuka amesema katika mkutano huo watapokea maoni hayo ambayo yatalenga kuonyesha wanataka Tanzania iweje katika miaka 25 ijayo kuanzia mwaka 2025 hadi 2050 ,kwa hiyo ni eneo muhimu sana kulite maoni
Amefafanua kwamba kwa sababu hawawezi kukusanya watu wote katika ukumbi huo wa halmshauri,basi watakusanya kwa makundi ya Viongozi hao niliowataja ,kwa hiyo kupitia Viongozi hao tunaomba Wananchi watoe maoni ili hao Viongozi waweze kuwasilisha katika mkutano huo
Tutakusanya maoni na kumpeleka ngazi zinazofuatia na maoni ya kwanza tutajadili tumetoka wapi na tunaelekea wapi na kikubwa tunachojadili ni Dira kulingana na maendeleao au mabadiliko ambayo yanatokea katika jamii yetu
Kuna mabadiliko ya kiuchumi ,kitekonolojia,kiufundi,mausiano na mabadiliko ya tabia Nchi ,hali ya hewa yote haya yanajumuhishwa katika dira na yatazingatiwa kwa hiyo ni vizuri yanapatikana maoni
Shabani Muhamedi makazi wa Sanya juu,amesma kukusanya maoni kuhusu Dira kwa makundi yote ikiwa ni pamoja na mwananchi mmoja mmoja niJambo jema sana kwa maendeleao ya Nchi
Mwisho
Mwisho