Na Richard Mrusha
Kampuni ya vifaa vya ujenzi FMJ hardware imeipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi kwenye sekta ya uwekezaji na biashara .
akizungumza leo na waandishi wa habari walipotembelea banda la serou kwenye maonyesho ya 48 ya kimataifa ya biashara 77 Jijini Dar es Salaam Afisa masoko,Jacqueline Yanga amesema wao kama wauzaji na wasambazaji wa vifaa vya ujenzi wamekuja kuonyesha bidhaa bora na zenye viwango vya hali ya juu.
Amesema serikali ya awamu ya sita imejipambanua kwa sababu imewapa wawekezaji hususan wazawa wigo mpana kwenye sekta ya uuzaji na usambazaji wa vifaa vya ujenzi .
Ameongeza kuwa FMJ hardware ni kampuni ya kizawa na ipo kwa ajili ya Watanzania wote na hata kwa nchi jirani kwa maana ya Afrika mashariki kwani inasambaza vifaa vya ujenzi kwenye hizo nchi za jirani.
Ameongeza wapo tayari kuwahudumia wananchi kipindi hiki cha 77 na hata baada ya 77 kwani ofisi zao zipo jijini Dar es laam Buguruni kisiwani.
“Ndugu wananchi wa Dar es laam na viunga vyake mnakaribishwa kwenye banda la serou kuja kujionea bidhaa bora kutoka FMJ HARDWAR “, amesema Jacqueline Yanga
Ameongeza kuwa kampuni hiyo inasambaza vifaa vya ujenzi kuanzia majengo hadi Madaraja.
Mwisho .