Na Mwandishi wa A24tv Arusha
Taarifa fiche kutoka vyanzo vya ndani zinaeleza kwamba ushiriki wa wachezaji wa Riadha katika mashindano ya Olympic ya mwaka huu 2024 Paris Nchini Ufaransa huenda kikosi Cha timu ya Tanzania iliyo tarajiwa kwenda kwenye mashindano hayo licha ya maandalizi ya safari na Mazoezi kwa wachezaji safari inaelezwa huenda ikawa imeota mbawa kufuatia uvumi kupitia mitandao ya kijamii na makundi ya Whatsapp ya wadau wa Riadha nchini.
Miongoni mwa taarifa zinabainisha kuwa dosari ya safari hiyo kusua sua ni kwasababu ya sintofahamu iliopo juu ya matumizi ya vifaa, vilivyo kabidhiwa katika Kambi hiyo hivi karibuni ikiwemo viatu,traki suti,fulana kutoka Kampuni ya Xtep.
Sintofahamu hiyo inatokana na mvutano uliopo kati ya Kamati ya Olimpic Tanzania ambayo ndio yenye maamuzi ya vifaa gani vitumike ambao inasemekana wao wameamua timu itumie vifaa vya kampuni ya Assics ya Japan wakati huo huo shirikisho la Riadha Tanzania likisisitiza kwamwa wanariadha wake watumie vifaa vya kampuni ya Xtep ya nchini China.
Taarifa hizo zinasema kwamba, Shirikisho la Riadha limetangaza bonus kwa wachezaji wake ya mamilioni ya fedha kwa kila medali watakayofanikiwa kuipata katika mashindano hayo. Bonus hizo ni za dola 50,000/- kwa medali ya dhahabu, dola 30,000/- kwa kila medali ya fedha na dola 20,000/- kwa kila medali ya shaba. Inasemekana wanariadha wamedhamiri kupambana ili kupata medali na kujivunia mamilioni hayo ya Xtep.
Kwa upande mwingine Kamati ya Olimpiki inasemekana imeshikilia msimamo wanariadha pamoja na wachezaji wa michezo mingine wote watatumia vifaa vya assics japo haijajulikana kama kuna faida yoyote ya kifedha ambayo wachezaji watapata kutokana na udhamini huo.
Mvutano kama huu uliwahi kujitokeza tena mnamo mwaka 2018 katika michezo ya Olimpiki iliofanyika Beijin China wakati ambao Shirikisho la Riadha lilikua na udhamini wa kampuni ya Lining lakini TOc iliwalazimisha kutumia vifaa vya kampuni ya Puma hali iliopelekea Shirikisho kuvunjiwa mkataba wake na Lining. Baada ya kuvunjika mkataba huo mwaka 2018 Riadha haikuwahi tena udhamini wa vifaa mpaka mwaka 2023 baada ya Kusainiwa mkataba na Xtep.
Taarifa za ndani kutoka kambi ya Riadha iliopo katika hotel ya Medan Jijini Arusha kwa udhamini wa CRDB Bank waliodhamini Riadha Tanzania zinasema wachezaji wako katika hali ya sintofahamu kwani wanaona donge nono la zawadi za Xtep zinaweza kuwaponyoka kama watalazimika kutumia vifaa tofauti na vya Xtep.
Tunatumai serikali itatusaidi ili tutumie xtep tuweze kulinda mkataba wetu kwakua huu mkataba ni wetu watu wa Riadha na unawasaidia wachezaji wengi wa timu za binafsi na za taasisi alisikika mdau mmoja wa riadha jijini Arusha akisema. Mdau huo aliongeza kua vifaa vya xtep vilisaidia hata timu ya jeshi la wananchi ilioshiriki mashindano ya Majeshi ya Dunia mwaka 2023 yaliofanyika nchini uswis.
Hadi tunakwenda mitamboni hatukufanikiwa kuwapata viongozi wa pande zote mbili ili kuweza kupata undani juu ya taarifa za jambo hili, endelea kufuatilia sakata hili na kufahamu hatma ya kikosi hicho ya Riadha kuelekea Ufaransa au kubaki Ardhi ya Tanzania.
Mwisho