Na Geofrey Stephen Arusha .
WAHASIBU wakuu wa Serikali wa nchi za bara la Afrika wapatao 2000 wanatarajiwa kushiriki katika Mkutano mkubwa wa pili wa kimataifa wa siku tatu,u utakaofanyika Desemba 2-hadi 5 mwaka 2024 kwenye kituo cha mikutano ya kimataifacha AICC Jijini Arusha.
Mhasibu Mkuu wa Serikali,CPA, Leonard Mkude,ameyasema hayo leo Jijini Arusha, alipokuwa akizungumza na Vyombo vya habari akielezea maandalizi ya Mkutano huo ambao utawashirikisha Wakaguzi Wakuu wa hesabu za Serikali barani afrika.
Mhasibu Mkuu wa Serikali,CPA, Leonard Mkude akiongea na vyombo vya habari .
Amesema kuwa lengo la mkutano huo uliandaliwa na Umoja wa Wahasibu Wakuu wa Serikali barani afrika ,AAAG,ni kujenga Imani ya Umma katika mifumo ya usimamizi wa fedha za umma kwa ukuaji endelevu wa uchumi kwa nchi za Afrika .
Amesema kuwa Mkutano huo utashirikisha Wahasibu,Wakaguzi wa hesabu ,wataalamu wa masuala ya fedha,Tehama ,Vihatarishi na kada nyingine wakiwemo Wahasibu kutoka Sekta binafsi..
Mkude,amesema kuwa Mkutano huo unafanyika kwa mara ya pili tangia kuanzishwa kwake Julai 5 mwaka 2023,ambapo mara ya kwanza ulifanyika Nchini Lesotho February 2024 .
Amesema kuwa Umoja huo ulizinduliwa Mombasa Nchini Kenya Julai 5 mwaka 2023,baada ya Azimio la kufunga Umoja wa Wahasibu waliokuwepo katika kanda mbalimbali wakifanya kazi kwa kutumia lugha za ukanda husika .
CPA,Mkude,amesema,Umoja huo upo chini ya Umoja wa nchi za Afrika,AU,kabla ya kuundwa kulikuwa na Umoja wa Wahasibu wanaozungumza lugha ya Kiarabu,Kiingereza,Kireno,Kifaransa hi yo ilikuwa ni vigumu kuelewana lakini sasa kupitia Umoja huo wamekuwa kitu kimoja
Amezitaja faida za Mkutano huo kuwa ni pamoja na Afrika yenye mafanikio yenye msingi wa ukuaji Jumuishi na maendeleo endelevu ,Bara Jumuishi lililounganishwa kisasa jwa kuzingatia maadili ya Pan-Africanism na maoni ya mwamko wa Afrika na Afrika yenye utawala Bora.
Faida nyingine ni uwepo demokrasia ,kuheshimu haki za binadamu na utawala wa Sheria ,Africa yenye amani na usalama ,Africa yenye utambulisho thabiti wa kitamaduni,urithi wa pamoja maadili na maadili yanauoshirikiwa.
Mkude,amesema kuwa sasa Umoja huo ni chombo kinachowaunganisha Wahasibu wote pamoja barani na kuwa na sauti moja ambapo Benki ya Dunia,Shirika la Global fund Finance, wamejitokeza kusaidia Umoja huo
Mwenyekiti wa Umoja huo wa Wahasibu Wakuu wa Afrika,Malehlohonolo Mahase kutoka Nchini Lesotho, amesema kuwa Mkutano huu unafanyika Nchini kwa ajili ya kujifunza kutokana na Tanzania kuwa kinara katika matumizi ya mifumo ya fedha.
Mwenyekiti wa Umoja huo wa Wahasibu Wakuu wa Afrika,Malehlohonolo Mahase
Amesema kuwa watajifunza zaidi kuhusu fursa za uwekezaji kwenye Utalii na maeneo mengine na Serikali inavyosimamia uchumi pia Nchini kuna demokrasia Amani na watu wake ni wakarimu sana na hivyo kuna vivutio vingi vya mbuga za wanyama .
Ataivyo amempongeza Mh Rais Samia Suluhu Hassan kwa kujali uzalendo na kudumisha amani kwa nchi yake pendwa ya Tanzania.
Aicc kwa upande wao wamesema wako tayari kupokea ugeni huo mkubwa na wako tayari kuwahudumia wagen hao na watapata fursa kutembelea vivutio vya mbuga za wanyama zinazo patikana katika mkoa wa Arusha .
Mwisho