Na Richard Mrusha
Mwenyekiti wa bodi ya PURA Halfan Ramadhani Halfani amesema wamejipanga vizuri kuongeza wawekezaji kwenye utafutaji kwani kwa mda mrefu walikuwa hawana wawekezaji wa kutosha
Amesema sasa hivi wanalo jukumu la kutafuta wawekezaji hususani kwenye hayo maeneo ambayo yako wazi ili kutekeleza hilo kwa sababu taasisi imekua ikifanya matayarisho.
Amesema sheria ya mafuta inasema wawekezaji watafutwe kwa njia ya ushindani na sio kwa kuokotwa na ili uwapate kwa ushindani kuna kitu kinafanyika kinaitwa Duru, Duru ni mkutano wa kutangaza maeneo husika ya miradi hivyo wanakuja pale kisha wanapewa utaratibu wa kuandika madokezo ya kuomba miradi.
Amesema na Duru hiyo inaweza kufanyika labda robo ya mwaka ujao na duru inakuwaje ukisoma Sheria ya mafuta ni kazi ya waziri kwasababu kutoa leseni ni kazi ya waziri na waziri akialikwa pale atakuja kumwaga sera na kuainisha huduma inayotolewa.
Aidha ameongeza kuwa PURA wanajukumu la kusimamia pale uuzaji wa gesi nje ya nchi utakapo anzishwa, kuna mradi serikali imekuwa ikizungumza kuwa inamuwekezaji ila mradi unaendelea vizuri kimazungumzo hususani kama mazungumzo yatafanikiwa basi wawekezaji wataweka mitambo pale Lindi, Likonko yakuchakata gesi.
“Sasa hapo litakuwa ni jukumu la PURA kusimamia uchakataji, uzungumzaji kuangalia masuala ya je Serikali inapata mapato yake halali katika hiyo shughuli” alisema Halfan.
Anasema kama msimamizi wa Sekta PURA anajukumu la kutunga sheria ndogo ya kuhakikisha kwamba sekta inafanya kazi kifanisi, kiusalama na kihalali.
Hayo ndio majukumu ya Pura kwa ujumla wake, nizungumzie miradi ambayo waliyo nayo kwa sasa Serikali amesema ni kuhakikisha kwamba wanaongeza wawekezaji kwenye utafutaji.
Mpaka sasa nadhani tunamaeneo ambayo yanazalisha gesi na yamekuwa yakizalisha gesi pale songosongo, wilaya ya Kilwa, na mnazi bei wilaya ya mtwara mjini, lakini mwaka huu serikali imetoa leseni ya uendelezaji ambayo ni hatua moja kabla ya uzalishaji.
Imetoa leseni kwa mwekezaji mmoja ambaye anatokea mtwara katika eneo linaloitwa Ntolia yule mwekezaji anaasili ya uarabuni, mategemeo atakuwa anaanza uzalishaji wa gesi hapo mwakani kwaiyo kwa sasa hivi atafanya matayarisho ya mwisho ambayo ni ujenzi wa bomba kutoka kwenye eneo la kisima kupeleka kwenye mitambo ya kuchakata gesi pale Madimpa, kama kilomita hamsini kutoka kusini mwa Mtwara.
“Tunategemea atakuwa na uwezo wa kuzalisha takribani futi za ujazo milioni mia moja kwa siku kiasi ambacho kinaweza kuongezeka hapo baadaye kwa kadri soko huku linapozidi kuimarika na kadri vile visima vitavyoweza kuonyesha uwezo wake wa kuzalisha, nazungumzia hilo kwa sababu kuna kitu kinaitwa curity suply huyu mwekezaji atakapoanza kuzalisha tukapata uhakika kwamba tutaendelea kupata gesi kwa ile mitambo tuliyoiweka hapa Tanzania kwa kipindi cha muda mrefu” alisema Halfan Halfan
Ameongeza kwamba kwa kipindi cha muda mrefu zaidi tunategemea gesi ile ya baharini ile ambayo itachakatwa pale Lindi na yenyewe watatupatia gesi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwa maana ya Nchini, pamoja na kwamba watakuwa wanauza kiasi flani watatakiwa kukiuza hapa Nchini.
“Kama PURA tumejipanga vizuri kuhakikisha kwamba hatutakuwa na uhaba wa gesi hiyo ndio dhana yetu, kwa kutafuta wawekezaji wapya kwa kuendelea kuwekeza” alisema Halfan Halfan.
Mwisho