Na Bahati Siha,
Waganga wa tiba asili na tiba mbadala Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro,wametakiwa kuwataja watu wanaofanya shughuli hizi bila kuwa na vibali ili Sheria iweze kuchukua mkongo wake
Pia kwa wale ambao vibali vyao muda wake unataka kumalizika wametakiwa kuviuisha tena
Haya yamesemwa na Mkuu wa Wilayani hiyo Christopher Timbuka,alipokutana na wahudumu hao wa tiba asili katika ukumbi wa Hospitali ya Wilayani hiyo,kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usalama katika wilaya hiyo.
Akizungumza katika kikao hicho Amewataka wahudumu hao kufanya kazi kwa mujibu na utaratibu unaokubalika na kwa mujibu wa vibali vyao
“Kubwa ni kufuata utaratibu zilizopo, nafahamu mratibu yupo hapa kuna namna ya usajili na baada ya muda vibali vile vinaisha muda wake na mnatakiwa kuviuisha”amesema Timbuka
Kubwa ni eneo la ulizi,ulinzi wa binadamu ,sisi Wenyewe ulinzi wa wenzetu na ulinzi wa mazingira yetu
Timbuka amesema lingine ni kupiga ramli kwamba mwizi akitokea naweza kumfahamu ,bahati nzuri sijasikia hilo ni kati ya vitu vinavyotia changamoto kwenye Nchi ,inafikia hatua mpaka mtu anakwenda kutoa suluhisho ambalo ukiangalia kalete viungo vya alibino ,kalete sehemu za siri
Sasa mambo kama hayo naomba sisi tuyakemee sana ,kwa sababu inatuharibia sifa ya waganga wa tiba asili na tiba mbadala.
Amesema hii itasaidia sana na tukifanya hivyo Serikali itakuwa na furaha kwemba inashirikiana kwenye swala la tiba mbadala tiba asili
Kikubwa kuwa na uaminifu kwa sababu wakati mwingine wanaibuka pia watu ambao hawaeleweki eleweki hawapo kwenye hiyo fani hawa ndiyo wanaharibu wanaingilia fani na wanaharibu sifa nzuri ya tiba asili na tiba mbadala
ulinzi Alibino alishambuliwa tukio hilo mmoja Hilo, sijui lilikuwa ni kutaka au kufanya Nini wakamjeruhi ,sasa vitu kama hivyo vinatuharibia sisi.
Uenda kuna mtu amejificha pahali anatangaza anatumia viongo vya alibino au sehemu za siri vitu kama hivyo
Amesema Watu kama hao inabidi tuwakemee na tutoe taarifa ,usigombane naye ,wewe toa taarifa kwenye mamlaka ,sisi tutashughulika naye,mtakuwa mmejitengenezea mazingira mazuri ya kufanya kazi kwa amani na serikali
Kama tulivyozungumza magonjwa mengine hatuna dawa , magonjwa kama ukimwi,kifua kikuuu na hata kisukari,tusaidieni katika hili kwamba ambao wanakuja kwenu na magonjwa ambayo hamuwezi kuyatibu basi ni vizuri sana yakaletwa kwenye Hospitali zetu ili waweze kupata tiba sahihi
Aidha katika kutunza mazingira , kama Serikali ni vizuri kama mtu anafahamu miti ya aina flani ile anayoitumia katika tiba basi tushirikiane na Taasisi za utafiti wa misitu au miti kuweza kupanda miti hii katika maeneo yenu hii ni kwa ajili ya kutunza mazingira
Hashimu Mtangi Mmoja ya Waganga hao,Amesema watakwenda kutekeleza yale yote waliusiwa na kutaka baadhi ya Viongozi wa Dini kuacha kuwasema vibaya kwamba wao wanausika katika kufanya mambo ya ukatili na kuomba kukutana nao ili kuelimishana zaidi kuliko kuwasema bila ya ushahidi.
Awali Peter Msaka mratibu wa jambo hilo wilaya ,amesema Wilaya hiyo ina Waganga wa tiba na tiba mbadala 16 kati yao 11 wamesajiliwa ,lakinj tumetaka wauhishe vibali kwa wale ambao vibali vyao vimefika mwisho
Mwisho