Na Bahati Siha,
Wananchi wa Kitongoji cha Makao mapya kata ya Orkolili Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro ,wamelalamika kuchoshwa na ahadi wanazopewa na Meneja wa I(TANESCO) Wilayani humo Ismael Salum kwamba watawekewa umeme ,
Ambapo wamesema huu mwaka wa 7 hawajapata licha ya nguzo kufika katika eneo.
Wakizungumza na waandishi wa habari katika Kitongoji hicho,wamesema jambo hilo limewaathiri kisakonolojia kwani wamekuwa wakiziangalia nguzo hizo kwa uchungu wa hali ya juu nakutamani bora zisingekuwepo
“Ni kweli huu ni mwaka wa 7 Nguzo kubwa zimesimamishwa hapo ,sasa kama waliona muda wa sisi kupata umeme hawajafika kwani hizi Nguzo walizileta hapa “walihoji Wananchi
Raphael Laizer,amesema kitendo cha kuzichimbia Nguzo hizo nakuingia mitini kimewafanya Wananchi hao kuwa na masikitiko makubwa ,na kusema wanapopiga simu Tanesco wanaambiwa wasubiri,sasa huu ni mwaka wa 7
Amesema baada ya kuziweka nguzo hizo waliwaeleza Wananchi kwamba kwenye nyumba waweke vifaa kwa ajili ya kupokea umeme, majumbani mwao ,vifaa hivyo waliekwenda kununua na mafundi waliwalipa fedha kwa ajili ya kutufungia vifaa hivyo
,”Nataka kuhuliza wakati wanazileta hapo nadhani walikuwa na uhakiki wa Wananchi kupata huduma hiyo kwa wakati,nataka kuhuliza changamoto hizo zitatuliwa lini,kwa sababu kila baada ya muda tukimpigia Meneja mwezi wa 7 hautavuka umeme utawaka”amesema Laizer
Giliadi Kawa katibu wa ccm tawi la Makao mapya ,ameomba Tanesco kumfikisha umeme mapema ili Wananchi waweze kufanya shughuli za maendeleao ikiwamo kuweka mashine za kusaga ,kufungua salon za kike na kiume pamoja na uchomeaji vyuma mbali mbali
Amesema kwa Sasa huduma za umeme wanazipata kwa maeneo ya mbali kwa kufanya safari ,wakati mwingine unapeleka simu kuchajiwa betri ya simu unabadilishiwa moja ya changamoto
Elisante Nasar, Mwenyekiti wa Kitogoji hicho ,amesema eneo hilo ambalo limebeba vitongoji viwili linawakazi zaidi ya 700,lakini cha kushangaza mpaka muda huu umeme haujawaka
Hata juzi Viongozi wa chama cha mapinduzi ( CCM),Wilaya walifika ndani ya tawi hili tuliwaeleza pia walimpigia simu Meneja wa Tanesco,tunaomba watusaidie nadhani Mama Samia Suluhuu Hassani Rais wetu atalisikia hili
Meneja huyo wa Tanesco Wilaya , amesema baadhi ya vitongoji wilayani humo Havina umeme moja wapo ni hicho kitongoji cha Makao Mapya,wavute subiri tutawafikia.
Hapo kinachosubiriwa ni Transfoma pamoja na nguzo dogo za kuingiza kule majumbani,
Sasa hicho kitongoji tumesha kuelekeza Rea ,tumewapelekea waweze kukihudumia,kwa hiyo naomba wavute subra ndiyo mwaka wa Serikali umeanza sasa
Mwisho