Na Richard Mrusha Dodoma
DODOMA: WAKULIMA nchini wameshauriwa kuitumia mbolea mpya aina ya UMKA ili kupata matokeo chanya katika kilimo.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Umka Afrika LTD inayojishughulisha na kuingiza mbolea nchini, Benjamin Laizer amesema hayo katika maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi yajulikanayo kama 88 yanayoendelea Jijini Dodoma.
Laizer amesema mkulima anapotumia mbolea hiyo hahitaji kuitumia nyingi kutokana na ubora wake.
“Mkulima anapotumia mbolea hii, anatumia mbolea kidogo kwa faida kubwa kwenye uzalishaji kwa sababu mkulima lazima aone tija.
” Kwenye kile ambacho unakitumia huhitaji kutumia kikubwa sana, unatumia kidogo ili upate kingi. Hii ndio faida tuliyonayo kama Umka,” amesema.
Kuhusu soko la mbolea, amesema hapa Tanzania mahitaji ni makubwa hivyo wao wana nafasi kubwa ya kuingiza bidhaa ambayo itakidhi mahitaji ya watanzania hususan katika kuongeza tija kwenye uzalishaji.
Mwisho