Na Mwandishi wetu Tanga
Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. Japhari Kubecha ametoa wito kwa Halmashauri ya Jiji la Tanga ◦ na mamlaka ya mapato (TRA) kufanya kazi kwa pamoja ikiwa ni pamoja na kuwezesha mifumo isomane ili kuokoa muda kwa wafanyabiashara. ◦ ◦ Mhe. Kubecha amesema hayo leo katika kikao cha wadau na wafanyabiashara ambapo amesikiliza kero mbalimbali za wafanyabiashara, wasafirishaji, wakulima, bodaboda, wadau wa viwanda, pamoja na wenyeviti wa masoko ya Jiji la Tanga.
◦ Kubecha amemwagiza Afisa Maendeleo ya Jamii Bw.Simon Mdende kutoa elimu kwa ◦ wafanyabiashara wadogo wadogo juu ya upatikanaji wa kitambulisho cha mfanyabiasha ◦○ ambapo imeonekana elimu ni ndogo kwa wananchi juu ya vitambulisho hivyo, huku akisisitiza G kuwekwa kwa utaratibu mzuri Wa utoaji mikopo kwa vijana ambao wametimiza vigezo na masharti juu ya mikopo.
‘Wekeni utaratibu wa kukutana na wafanyabiashara kila baada ya miezi mitatu, lengo likiwa ni kutataua changamoto za wafanyabiashara lakini pia wafanyabiashara tulipe Kodi”.Amesema Kubecha.
Aidha katika kikao hicho Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Mhandisi Juma Hamsini amewatoa hofu wafanyabiashara juu ya ujenzi wa masoko ya MIlango wa Chuma, Mgandini, Makorora na ukarabati wa soko la Ngamiani kwamba kazi hiyo itafanyika.
Mwisho