GEofrey Stephen ARUSHA
MTANDAO wa Watetea wa haki za binadamu Tanzania(THRDC)umeomba kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuzungumzia hatima ya masuala ya utekaji na ukatili yanayoendelea nchini pamoja na kumkumbusha mikataba ya kimataifa ya kupinga ukiukwaji wa haki za binadàmu.
Akiongea na vyombo vya habari katika mkutano mkuu wa 13 wa wanachama wa mtandao THRDC unaoendelea katika wiki ya AZAKI jijini Arusha,
mratibu wa Taifa wa Mtandao wa kutetea haki za Binadamu, Onesmo Ole Ngurumwa alisema mkutano huo umelenga kuangazia masuala mbalimbali ikiwemo kupitia na kuidhinisha taarifa ya nusu muhula ya hali ya haki za binadamu ,utekelezaji wa mapendekezo ya kipindi kilichopita.
“Tumekutana hapa kwa ajili ya kupitia na kuidhinisha taarifa ya nusu muhula kuhusu hali ya haki za binadamu katika kuangalia utekelezaji wa mapendekezo,pamoja na kuketi na wafanyabiashara wenye makampuni ya kibiashara Tanzania ambao wanaweza kutuunga mkono kupitia rasilimali fedha katika mapambano ya utetezi wa haki za binadamu kuhusu ukatili”.
Alisema wadau wa haki za binadamu wamekuwa na changamoto kubwa katika kupambana na utekeji mauaji na ukiukwaji wa haki za binadamu na hivyo wameomba kukutana na Rais Samia ili kuona namna ya kupata suluhu ya kukabiliana na changamoto hizo zinazogharimu maisha ya watu.
“Tulitoa mapendekezo yetu kwa rais Samia kuhusu uundaji wa tume rasmi ya kiraia ya kudumu inayohusisha watu wengi na tulimshauri aridhie mikataba miwili ya kimataifa inayopinga masuala ya utekaji na ukatili na ndio maana leo tumeadhimia kwenda kukutana naye baada ya miaka mitatu kupita ”
Alisema mkutano huo wenye ajenda ya Kuboresha namna ya kupata Rasilimali za ndani,unalenga kumshawishi rais aridhie kusaini mikataba miwili ya kimataifa inayopinga masuala ya ukatili nchini.
Raphael Maganga Mkurugenzi Mkuu taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPCF),alisema jukumu kubwa la sekta binafsi ni kuona namna inayoweza kushirikiana na taasisi mbalimbali kukuza utetezi wao katika haki za binadamu.
Alisisitiza kuwa sekta binafsi zinawajibu wa kutetea haki za binadamu kama watoto,vijana na wanawake katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa uhuru na ufanisi zaidi.
Alisema taasisi za kutetea haki za binadamu zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa ila zinapaswa kuwa imara na kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi ili kuhakikisha jamii yote inakuwa na haki sawa.
Ends…